Katika kuboresha na kufanya maisha ya Watanzania kuwa murua, Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii”Vodacom Foundation”, imekabidhi msaada wa vitu mbalimbali na vyakula wenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 29 kwa kituo cha walemavu mbalimbali wakiwemo wenye ulemavu wa ngozi, Albino, kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Akikabidhi msaada huo kwa uongozi wa kituo hicho, Kaimu Mkuu wa Vodacom kanda ya Tanganyika, Sabas Ademba amesema kampuni hiyo imeamua kusherehea sikukuu ya mwaka mpya 2016 kwa kuijali jamii ya watu wenye mahitaji muhimu hapa nchini.
Zoezi la msaada huo unaotolewa kupitia kampeni maalum ijulikanayo kama Pamoja na Vodacom inayotoa misaada mbalimbali wakati wa msimu wa sikukuu itafanyika nchi nzima huku kituo hicho kimenufaika na jozi za viatu, soksi, fulana, masweta, sare za shule, Kofia pana kwa ajili ya kujizuia na jua, shuka na vyandarua,Vingine ni madaftari, kalamu seti za hesabu, sabuni, dawa za meno, vifaa vya usafi kama mafagio na dawa za vyooni huku upande wa chakula ni pamoja na mchele, Unga, maharagwe, mafuta ya kupikia na Chumvi..
Katika hatua nyingine wahudumu wa afya wa zahanati iliyopo katika kituo hicho wamesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa dawa zinazohitajika kwa matibabu ya watoto hao wenye ulemavu wa ngozi.Wakizungumza na waandishi wa habari wahudumu hao wa afya wamesema watoto hao wanakabiliwa na magonjwa ya aina mbalimbali ikiwemo kukumbwa mara kwa mara na magonjwa ya Ngozi, Kuhara, U.T.I na Minyoo.
Grace Lali anasema kufuatia kuwepo kwa magonjwa hayo zahanati hiyo imekuwa ikikabiliwa na ukata wa dawa za kuwahudumia hali ambayo imewafanya kulifikisha suala hilo kwa mganga mkuu wa manispaa ya Shinyanga ili hatua zaidi zichukuliwe,
Aliipongeza Vodacom Foundation kwa kuwajali watoto hao na anatoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano wa mfuko huo hivyo anawaomba watu binafsi, asasi za serikali na zisizo za serikali, mashirika na makampuni kujitokeza kuwasaidia madawa ili watoto hao waweze kukua katika afya njema.
Naye Felister John, muuguzi katika kituo hicho amesema watoto hao wanakabiliwa na uhaba vitamini A, kutokana na kula chakula cha aina moja tu, ya wanga, ambavyo ni ugali, ubwabwa na maharage.
"Watoto hawa wanahitaji matunda, vyakula bora kama nyama, maziwa ambavyo ni adimu sasa kukosekana na kwa vitu hivyo kunawafanya kuwa wadumavu" Alisema Felister John.
Mkuu wa kituo hicho Peter Ajali, anasema misaada wanayoipata ikiwemo iliyotolewa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom unasaidia kupunguza makali ya uhitaji wa watoto hao.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa kituo cha Buhangija chenye watoto takribani 400, kinaendeshwa kwa kutegemea misaada kutoka kwa wahisani kwa kuwa serikali inawahudumia watoto 40 tu kwa kufuata takwimu za zamani.
Mwisho.
Baadhi ya watoto wenye ualbino wanaolelewa katika kituo maalum kilichopo katika Manispaa ya
Shinyanga mjini wakiwa katika hafla fupi ya kukabidhiwa msaada wa vifaa mbalimbali vya michezo na vyakula
wenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni
29 uliotolewa na Vodacom Foundation kwa ajili ya sikuu ya mwaka mpya na
kukabidhiwa na Kaimu Mkuu wa Vodacom Tanzania wa kanda ya Tanganyika,Sabas
Ademba(hayupo pichani)
Kaimu Mkuu wa
Vodacom Tanzania kanda ya Tanganyika,Sabas Ademba akiongea na watoto
wenye ulemavu wa Ngozi”Albino”wanaolelewa katika kituo maalum kilichopo katika
Manispaa ya Shinyanga mjini wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa msaada wa vifaa mbalimbali vya michezo
na vyakula wenye thamani ya zaidi ya
Shilingi milioni 29 uliotolewa na Vodacom Foundation,kupitia program
yake ya Pamoja na Vodacom kwa ajili ya sikuu ya mwaka mpya.
Mkuu wa kituo
maalum cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi cha Manispaa ya Shinganga,
Peter Ajali(kushoto)akikabidhiwa moja ya msaada wa vifaa mbalimbali vya michezo na vyakula vyenye
thamani ya zaidi ya Shilingi
milioni 29 na Kaimu Mkuu wa Vodacom
Tanzania wa kanda ya Tanganyika,Sabas Ademba(kulia)uliotolewa na Vodacom
Foundation kwa ajili ya sikuu ya mwaka mpya.
Ni vyema Serikali kuonyesha uongozi madhuburi katika kuwahudumia ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi. Ni sahihi kushirikiana na Chama cha Watu wenye ualbino nchini ili tusiwape nafasi wageni wanaotaka kufanya hivyo kwa lengo tu lakujitafutia umaarufu wao binafsi huko nje ya nchi.
ReplyDeleteKwanini tunawatenga na kuwaweka peke yao hawa watoto? Mie napendekeza wachanganywe na watoto wengine wa kawaida. Mie tulivyokuwa tunasoma shule ya msingi/secondary/chuo kikuu tulikuwa na hawa ndugu zetu. Tunavyowaweka (segregate) hivi inaleta picha mbaya na hata wao wenyewe wanaweza kujihisi kuwa wapo tofauti au hawawezi kufanya vitu kama watu wengine, ambayo sio kweli.
ReplyDelete@Msemakweli umeonesha namna ulivyo Na mapenzi Na ndugu zetu hawa,ila nakukumbusha Tu hili la kuwekwa hawa ndugu zetu pmj huenda Kuna sababu za msingi,km upo ndani ya nchi unaweza tembelea kanda ya ziwa yote Na ukaanza research ya ugumu wa maisha Na kukosekana usalama kwa watu wa aina hiyo,pia waweza uliza tu km hutoweza fika huko,la km upo nje ya nchi basi nikujuze Tu njia ya haraka Ili kunusuru maisha ya watu hawa kwanza Ni mfano wa hii ilofanywa,kuwa Na vituo maalum vya kuwakusanya Na kuwahudumia Na kuwa chini ya uangalizi maalum mpk pale njia mbadala itakapopatikana. Kwanini?sababu kuu Ni Ile haki ya msingi ya kila raia wa Tanzania "kuishi kwa uhuru Na usalama" hili limekosekana kwa ndugu zetu hawa ,wamekua wakiishi kwa khofu kuu dhidi ya watu wenye malengo Yao hasa yakihusishwa Na ushirikina ,huwakamata Na kuwakatakata mapanga Na kuwaua Na kutoroka Na viungo vya miili Yao.hili Ni mambo haya kabisa ktk nchi huru Kama yetu.kuwanusuru serikali Na washika dau mbalimbali wakaplan kitu Kama centers Ili wawe chini ya mikono salama .na imani serikali hii itakuja Na ufumbuzi rasmi.ni matukio mengi yameripotiwa ya kuuliwa Na kujeruhiwa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi hasa mikoa ya Kati Na kanda ya ziwa.
ReplyDelete