TAARIFA
KWA UMMA
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali anakusudia
kuyachukulia hatua Mashirika yanayoendesha shughuli zao kinyume cha Sheria ya
NGOs Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa mwaka 2005.
Mashirika hayo ni
yale ambayo hayajawasilisha taarifa za mwaka kwa kipindi cha miaka miwili
pasipo kutoa sababu za msingi, kulipa ada ya mwaka au kuendesha shughuli za
NGOs bila kusajiliwa chini ya Sheria ya NGOs.
Kwa taarifa hii, Mashirika husika yanatakiwa yawe
yamerekebisha dosari tajwa ndani ya siku thelathini (30) kuanzia tarehe ya
tangazo hili. Baada ya kipindi hicho, Msajili wa NGOs atayafutia usajili
Mashirika ambayo yatakuwa hayajawasilisha taarifa na kuyachukulia hatua stahiki
Mashirika yanayoendesha shughuli za NGOs bila ya usajili chini ya Sheria
husika.
Malipo yote ya ada yafanyike kupitia Benki ya NMB, NGO Account Na. 20110014074 na stakabadhi halali ya
malipo itumwe kwa Msajili wa NGOs.
Imetolewa na:
M.S. Katemba
MSAJILI
WA NGOs
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,
JINSIA, WAZEE NA
WATOTO
06 Januari, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...