Bondia Geoger Dimoso akisaini mkataba wa kuzipiga na Abdallah Pazi wa pili kushoto kulia ni mlatibu wa mpambano huo Pembe Ndava na kushoto ni kocha Mbaruku Heri

Mabondia Georger Dimoso (kushoto)  wakitunishiana misuli na Abdallah Pazi wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika March 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa Pwani katikati ni mratibu wa mpambano uho Pembe Ndava Picha na SUPER D BOXING NEWS

MABONDIA Abdallah Pazzi na Georger Dimoso wamesaini mkataba wa kuzipiga Bagamoyo mkoa wa Pwani March 5 katika uzito wa kg 74.

Akizungumza wakati wa kutiliana saini Promota wa mpambano uho Muhusin Sharif amesema kuwa wameamua kupeleka mpambano uho Bagamoyo kwa ajili ya wakazi wa mkoa wa pwani wapate burudani ya masumbwi siku hiyo.
Aliongeza kwa kusema kuwa anaomba makampuni mbalimbali kutoa sapoti kwa ajili ya udhamini wa mapambano hayo kwa kuwa Bagamoyo mchezo huo unapendwa na ndio unachipukia hivyo anaomba sapoti kwa makampuni na taasisi mbalimbali kusaidia mchezo uho ili uendelee kukua hapa nchini.

"Bagamoyo hatuna jukwaa 'ring' la ngumi hata moja mpaka tukodishe kutoka Dar es salaam yaje hapa ndio vijana wapate kucheza. "Hivyo naomba wadau mbalimbali wajitokeze kuchangia upatikanaji wa jukwaa hilo ili  mchezo wa ngumi usonge mbele hapa" alisema.

Siku hiyo mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo bondia Sadiq Momba atakumbana na Baina Mazola katika uzito wa kg 59 na Adam Yahaya atakumbana na Selemani Bagaiza katika uzito wa kg 49 na Juma Khan atapambana na Bruno Vivuaviwili na Abdallah Zamba atakumbana na Twalibu Tuwa.
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi.
Pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...