Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mama Juliana Yassoda akifunga kozi ya
ukocha wa wanawake ngazi ya juu (High Level Course) iliyoandaliwa na TFF kwa
kushirikiana na FIFA.
Akiongea wakati wa kufunga kozi
hiyo, Mama Yassoda amesema anaishukuru TFF/FIFA kwa kuona wanawake wanapata
nafasi ya kushiriki kozi mbalimbali, ikiwemo kozi hiyo ya ukocha kwa ngazi ya
juu kwa wanawake.
Mama Yassoda amewataka
washiriki wa kozi hiyo kuyafanyia kazi mafunzo waliyopatiwa katika kuhamasisha
wanawake wengi kuupenda mpira wa miguu na kuzalisha vipaji vya wachezaji wengi
wa kike kuanzia ngazi za chini, na sio kuhitimu na kuweka vyeti ndani tu.
Naye Mariam Mchaina akiongea
kwa niaba ya washiriki wenzake, ameishukuru TFF kwa kuwakumbuka wanawake na
kuwapatia kozi hiyo ya ukocha, na kuahidi watakaporudi sehemu wanazoishi
watatumia ujuzi walioupata kufundisha wanawake mpira miguu kwa ngazi zote.
Kozi hiyo ya ukocha kwa
wanawake, ilianza Jumatatu na kumalizika leo ambapo jumla ya washiriki 25
wameshiriki kozi hiyo ya awali kutoka katika mikoa ya Dar es salaam, Iringa,
Ruvuma, Pwani na Tanga na kupewa vyeti ya ushiriki na mpira kama kifaa cha
kuanzia kazi ya ukocha.
Picha ya pamoja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...