MWIGIZAJI na mchekeshaji wa nchini Kenya, Eric Omondi amewasili mchana huu jijini Dar leo akiwa na kikosi kazi chake wakiwa tayari kwa 'LIVE SHOW' kesho katika ukumbi wa mikutano wa Marqee uliopo hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam.
Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi akiwa na kikosi kazi chake wakiwasili katika jengo la Alosco Tower lililopo Lumumba jijini Dar es Salaam leo.

Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi akiwa katika pozi na bango la GSM Media leo alipo wasili jijini Dar es Salaam kwaajili ya 'LIVE SHOW' itakayofanyika kesho katika hoteli ya Hyatt katika ukumbi wa Marqee jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi akiwa na Meneja Mkuu wa GSM Media, Deo Ndejembi (katikati) na Dj wa mchekeshaji huo, wakiwa katika ofisi cha GSM Media leo mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa GSM Media, Deo Ndejembi na Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi wakiwa katika picha na kikosi kazi cha mchekeshaji huyo ambapo 'LIVE SHOW' itakayofanyika kesho jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...