Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kuachia wimbo  Jumatano hii anajipanga kuachia wimbo mpya uitwao 'Sizonje' akiwa amemshirikisha msanii kutoka B Band, Banana Zorro.

Akizungumza na mwandishi wetu Jumatatu hii, Mpoto alisema kazi hiyo iliyotayarishwa katika studio yake chini ya producer Allan Mapigo, ni kazi bora ambayo itakonga mioyo ya mashabiki wake.
“Nimefanya kazi ambayo kila mtu akiisikiliza atatoka na kitu chake kwa sababu ni kazi ambayo nimetumia muda mwingi kuiandaa,” alisema "Sizonje ambae namzunguzia kwenye hii nyimbo ni mtu, yaani hawa wewe kwenye kazi yako, nyumbani, hospitali unaweza ukawa Sizonje. Kwahiyo ni wimbo ambao kila mtu akiusikiliza atatoka na kitu,",
Aliongeza “Hii kazi ni yule Mrisho Mpoto wa  Nikipata Nauli, Kazi ambayo mpaka leo mtu akisikiliza anatamani zaidi kuendelea kusikiliza ili aelewe nini kinaendelea kwenye hii dunia,”.
Mrisho Mpoto na Banana Zoro waliwai kufanya kazi ya pamoja ya wimbo ‘Nikipata Nauli’ ambayo ilifanya vizuri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...