Na Nyakongo Manyama-MAELEZO


Mkoa wa Mwanza unatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa kumwombea Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Taifa kwa ujumla.

Maombi hayo yanatarajiwa kufanyika Jumatano ya wiki ijayo katika Viwanja vya Furahisha. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa  Good News For All Ministry  Askofu Dkt.Charles Gadi wakati wa mkutano wake na waandishi wa wahabari leo jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa wanachukua fursa hiyo kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wasaidizi wake kwa kutambua kazi nzuri anayoifanya ya kupambana na ufisadi na kuleta maendeleo ya nchi na watu wake.

Askofu huyo ameongeza kuwa sanjari na maombi ya kuwaombea viongozi , pia wataiombea Tanzania ili iepukane na majanga mbalimbali kama vile ukame, njaa na mvua za el-nino ambayo yanaweza kusababisha maafa kwa  wananchi.

Ameongeza kuwa katika maombi hayo mkutano utapata fursa ya kutubu na kumwomba Mungu alete mvua za kusaidia wananchi na wanyama wa kufugwa na wa mwituni.

 “Tutamwomba Mungu ili nchi yetu ijitosheleze kwa chakula na pia iweze kuuza  akiba nje na kutuletea fedha za kigeni” alisema Askofu Dkt Gadi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. KUMUOMBEA JPM NI KILA MTU KUFANYA KAZI KWA BIDII NA UFANISI ZAIDI. SIO KILA KUKICHA WATU WANAACHA KAZI NA KUJUMUIKA VIWANJANI. MATHALANI KAMA WATAKUJA WATU 1000 SI KAZI KUBWA INGEFANYIKA? KAZI KAZI KAZI.HAKUNA KUTAFUTA VISINGIZIO VYA KUACHA KAZI NA KULA PESA ZA WANAOFANYA KAZI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...