Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (kulia) akimsalimia Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile wakati alipowasili Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Masauni aliiagiza Idara hiyo kuchunguza Makapuni yanayotoa ajira kwa wageni ambapo ajira hizo wangepewa Watanzania wenye sifa na kupunguza tatizo la ajira nchini.
 Kamishna wa Idara ya Uhamiaji (Utawala na Fedha), Piniel Mgonja akitoa taarifa fupi ya utendaji wa Idara hiyo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (katikati) wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (wanne kushoto), Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile (wanne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji. Naibu Waziri Masauni alifanya ziara ya kikazi katika idara hiyo kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na idara hiyo. Hata hivyo, katika hotuba yake, aliiagiza idara hiyo kuchunguza Makapuni yanayotoa ajira kwa wageni ambapo ajira hizo wangepewa Watanzania wenye sifa na kupunguza tatizo la ajira nchini .
 Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ndugu michuzi naomba nitoe hili dukuduku langu la moyo. Mimi Ni makazi wa UK London passport yangu imeisha muda wake hivyo nimeenda kutengeneza mpya hapo Ubalozi wa Tanzania London. Imechukua miezi 9 hamna chochote kilicho fanyika. Jibu likaja kuwa hawawezi kutoa passport mpaka nipeleke cheti cha kuzaliwa cha baby yangu au bibi yangu sasa Mimi Nina miyaka 41 sasa bibi yangu sijawahi hata kumuona wala bibi hivyo Mimi nitavitoa wapi vyeti vyao vyao vya kuzaliwa pengine hata hawana. Nimepeleka cheti changu cha kuzaliwa vyeti vya baba Na mama yangu vyote vya kuzaliwa nimekamilisha kila kitu vinavyo hitajika kisheria Ili niweze kupata passport. Hivyo tutolee haya mbambo wazi Ili Kama Kuna ufisadi wowote ule upo halo wizarani ubainike.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...