Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini, Lu Youqin akizungumza katika kikao na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Mhe. Charles Kitwanga (wa pili upande wa kushoto).  Katika kikao hicho kilichofanyika Wizara hapo, viongozi hawa walijadili masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano wa Serikali ya China na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga (wa kwanza upande wa kulia), akimsikiliza Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Lu Youqing (wapili upande wa kushoto) wakati wa mazungumzo yaliyohusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati Serikali ya China na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Mazungumzo hayo yalifanyika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam..
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia), akizungumza na ujumbe wa Ubalozi wa China  nchini Tanzania, ulioongozwa na Balozi LuYouqing, (hawapo pichani), katika mkutano uliojumuisha pande hizo mbili kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali ya Watu wa China na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
 Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Lu Youqing , akisaini kitabu cha wageni mara baadaya kuwasili katika Ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia), ofisini kwake alipowasili Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa ziara fupi. 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wa nne kutoka kulia), akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania, ulioongozwa na Balozi Lu Youqing (watatu kutoka kulia). Ujumbe huo ulitembelea Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kujadili masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.(PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...