Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (katikati) akizungumza na Machifu wa kisukuma kwenye kituo cha Utamaduni Bujora, kulia pichani ni Jaji Mstaafu Mark Bomani na kushoto ni Chifu Charles Kafipa wa Bukumbi mkoani Mwanza.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amesimikwa uchifu wa kisukuma mara baada ya kutembelea kituo cha utamaduni wa kisukuma cha Bujora.
Katika tuzo hiyo ya watemi wa kisukuma ambayo risala yake imeandikwa na kusainiwa na Katibu wa Umoja wa Watemi wa Kisukuma Mtemi CM. Dotto Itale, wamemtakia heri na kumuomba mwenyezi mungu amsaidie kufanya kazi zake vizuri na kumtunukia cheo cha Manju Mkuu kiongozi wa ngoma kubwa mwenye kughani umati wote ukaitikia, na kumpa jina la Sangija ambalo linaunganisha Mamanju wote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...