Matukio ya Wizi wa Maji yamekuwa yakikithiri kila kukicha katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam licha ya hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Mamlaka husika za kisheria pindi mtu au kikundi cha watu kinapobainika kufanya ubadhirifu huo.

 Shirika la majisafi na Majitaka Dar es salaam(DAWASCO), imewakamata raia 2 wa china ambao  wamejiunganishia huduma ya Maji kinyume na taratibu katika eneo la Buguruni Jijini Dar es salaam, katika godauni moja inayomilikiwa na kampuni ya ALLIED TRANSPORT, jengo ambalo wachina hao wamepanga huku wakiendesha shughuli zao za utengenezaji wa mabati.

Kampuni hiyo ya wachina inayojishughulisha na utengenezaji wa mabati imebainika kujiunganishia huduma hiyo na Meneja wa Dawasco Wilaya ya Ilala Mhandisi Ramadhani Mtindasi wakati wa msako mkali ulioanza katika wilaya yake ya kuwabaini wahujumu miundo mbinu ya Maji na wezi wa Maji.

Mhandisi Mtindasi amesema kuwa matukio ya Wizi wa Maji kwa wilaya ya Ilala yamekidhiri sana na yanapelekea adhari kubwa sio tu kwa shirika bali hata kwa watumiaji wa Maji waliopo eneo la Ilala kutokana na Maji mengi kuishia mikononi mwa wachache hivyo kupelekea uhaba na kero ya Maji kwa maeneo yenye stahili ya Maji.


BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...