Wakati Taifa na Mataifa yakiendelea kutoa pongezi zao kwa serikali ya Rais.J.P.Magufuli kwa speed yake ya kuchapa kazi,Mawaziri wake pia wameendelea kuonesha namna walivyodhamiria kusimamia shughuli za maendeleo ya Nchi yetu.

Hii leo,Mh:Mwigulu Nchemba mwenye dhamana ya Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi amefanya ziara ya siku moja kwenye ranchi ya Taifa ya Ruvu kukagua ujenzi wa majengo ya machinjio ya kisasa ulioanza mwaka 2010.

Katika hali ya kusikitisha na kulazimu kuchukua hatua za kinidhamu,Mwigulu Nchemba amekutana na ubadhilifu wa Bilioni 5.7 ambazo zilitolewa kwaajili ya ujenzi wa jengo hilo,Fedha hizo zilizokuwa zimelengwa kuwezesha ujenzi wa machinjio hayo ya kisasa hazijafanya kazi kama ilivyokusidiwa.

Waziri huyo wa kilimo amekuta mradi huo umetelekezwa tangu mwaka 2010 bila kuendelezwa,Sababu za kutelekezwa kwa mradi huo zikidaiwa kuwa ni kutofautiana kwa mkandarasi na bodi ya NARCO(kampuni ya usimamizi wa ranchi za Taifa) hazikukubalika na Mh:Mwigulu Nchemba ambaye baada ya kusikiliza kwa makini ufafanuzi wa kutoka kwa viongozi wa ranchi hiyo aliamua ifuatavyo.

Kwanza,Mwigulu Nchemba amewatimua wakurugenzi wote wa bodi ya NARCO yenye dhamana ya kusimamia ranchi za Taifa kwa kushinda kukamilisha ujenzi wa mradi huo.Mbali na kushindwa,bodi hiyo imeutelekeza mradi huo na hivi sasa inapendekeza kujengwa kwa mradi mwingine kama huo ndani ya eneo hilohilo la ranchi ya ruvu.

Pili,Mwigulu Nchemba amesitisha utumishi wa Mkurugenzi mkuu wa ranchi za Tiafa kwa kushindwa kuchukua hatua za kusimamia ujenzi wa mradi huo hadi kukamilika kwake.

Pia,waziri huyo wa kilimo ameagiza kupitia vyombo vya sheria,wahusika wote walioshiriki ama kwa makusudi au kwa njia yoyote kuhujumu mradi huo usifanikiwe wanachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo.

Mwisho,Nchemba amewaagiza wataalam wa wizara yake kuhakikisha ndani ya siku 7 wanampelekea ripoti ya thamani ya jengo lililokwisha kujengwa na fedha zinazotakiwa kumalizia ujenzi wa jengo hilo.

Sambamba na hatua hizo,Mwigulu ametoa rai kwa watumishi wote wa umma kuwa mstari wa mbele kusimamia kwa ufanisi na uzalendo miradi yote ya maendeleo ya nchi yetu,Mbali na hapo,serikali ya Magufuli haitakuwa tayari kuona mali ya umma inachezewa na kuibiwa wakati kuna watanzania wanaweza kusimamia mali hizo na kuziendeleza.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi akiwasili kwenye mradi uliodumaa wa Ujenzi wa machinjio ya kisasa wa ranchi ya Ruvu mapema hii leo.Sehemu ya jingo lililobaki kama Gofu mara baada ya kutelekezwa na Uongozi wa Bodi ya ranchi za Taifa(NARCO)Mwigulu Nchemba akishangaa namna mali hii ya Umma ilivyotekelezwa.Mwigulu Nchemba akiwa na Mbunge wa Chalinze Mh.Ridhiwani wakisikiliza kwa makini sababu zilizopekea jingo hilo kutelekezwa.Anayetoa maelezo wa mwisho kushoto ni msimamizi wa ranchi hiyo Ngd.Bwire.Mwigulu Nchemba akiendelea kupewa maelezo ya kina kuhusu ubadhilifu uliojitokeza kwenye ujenzi huu.Picha/maelezo na Festo Sanga Jr.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Tatizo kubwa si kuelewana kati ya mwekezaji na wananchi wanauzunguka hiyo ranchi ila ni hao wahuni kutumia vibaya fedha za ujenzi na kuacha ujenzi katika hiyo hali ya kusikitisha. Nilitegemea wahusika wote kuwa wameshakamatwa na wapo wanaozea magerezani lakini bado tu waziri anaendeleza maneno na maonyo ambayo kwa muda huu hauhitajiki zaidi ya "action". ACTION SPEAK THAN WORDS. Kila mradi ukiiba billion 5.7 tutakuwa tunaenda mbele au tunarudi nyuma??? NI KIASI GANI KINAIBIWA KAMA MRADI MMOJA TU WATU WANAIBA KIASI HICHO????

    ReplyDelete
  2. There is a time when the government will sack everybody - the country has been rotten for a long time and It is very very hard to clean it by timua timua. Lock them up.

    Make them political detainees then courts will not free them.

    ReplyDelete
  3. How about the previous Ministers who were responsible in overseeing all that shit. They should be accountable!!

    Hawa nivifaranga tu, majogoo watoto wao wanaishi ulaya etc etc

    ReplyDelete
  4. Hongeraa mheshimiwa kwa kazi yako, lkn nauliza hivi, hizo Fedha ziloliwa jee? Na Hao walokula hizo fedha watachukuliwa hatua gani ili kurudisha? Maana ushaagizwa zifanywe hesabu za kutolewa nyengine

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...