Wakati
Taifa na Mataifa yakiendelea kutoa pongezi zao kwa serikali ya
Rais.J.P.Magufuli kwa speed yake ya kuchapa kazi,Mawaziri wake pia
wameendelea kuonesha namna walivyodhamiria kusimamia shughuli za
maendeleo ya Nchi yetu.
Hii
leo,Mh:Mwigulu Nchemba mwenye dhamana ya Wizara ya Kilimo,Mifugo na
Uvuvi amefanya ziara ya siku moja kwenye ranchi ya Taifa ya Ruvu kukagua
ujenzi wa majengo ya machinjio ya kisasa ulioanza mwaka 2010.
Katika
hali ya kusikitisha na kulazimu kuchukua hatua za kinidhamu,Mwigulu
Nchemba amekutana na ubadhilifu wa Bilioni 5.7 ambazo zilitolewa
kwaajili ya ujenzi wa jengo hilo,Fedha hizo zilizokuwa zimelengwa
kuwezesha ujenzi wa machinjio hayo ya kisasa hazijafanya kazi kama
ilivyokusidiwa.
Waziri
huyo wa kilimo amekuta mradi huo umetelekezwa tangu mwaka 2010 bila
kuendelezwa,Sababu za kutelekezwa kwa mradi huo zikidaiwa kuwa ni
kutofautiana kwa mkandarasi na bodi ya NARCO(kampuni ya usimamizi wa
ranchi za Taifa) hazikukubalika na Mh:Mwigulu Nchemba ambaye baada ya
kusikiliza kwa makini ufafanuzi wa kutoka kwa viongozi wa ranchi hiyo
aliamua ifuatavyo.
Kwanza,Mwigulu
Nchemba amewatimua wakurugenzi wote wa bodi ya NARCO yenye dhamana ya
kusimamia ranchi za Taifa kwa kushinda kukamilisha ujenzi wa mradi
huo.Mbali na kushindwa,bodi hiyo imeutelekeza mradi huo na hivi sasa
inapendekeza kujengwa kwa mradi mwingine kama huo ndani ya eneo hilohilo
la ranchi ya ruvu.
Pili,Mwigulu
Nchemba amesitisha utumishi wa Mkurugenzi mkuu wa ranchi za Tiafa kwa
kushindwa kuchukua hatua za kusimamia ujenzi wa mradi huo hadi
kukamilika kwake.
Pia,waziri
huyo wa kilimo ameagiza kupitia vyombo vya sheria,wahusika wote
walioshiriki ama kwa makusudi au kwa njia yoyote kuhujumu mradi huo
usifanikiwe wanachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo.
Mwisho,Nchemba
amewaagiza wataalam wa wizara yake kuhakikisha ndani ya siku 7
wanampelekea ripoti ya thamani ya jengo lililokwisha kujengwa na fedha
zinazotakiwa kumalizia ujenzi wa jengo hilo.
Sambamba
na hatua hizo,Mwigulu ametoa rai kwa watumishi wote wa umma kuwa mstari
wa mbele kusimamia kwa ufanisi na uzalendo miradi yote ya maendeleo ya
nchi yetu,Mbali na hapo,serikali ya Magufuli haitakuwa tayari kuona mali
ya umma inachezewa na kuibiwa wakati kuna watanzania wanaweza kusimamia
mali hizo na kuziendeleza.
Tatizo kubwa si kuelewana kati ya mwekezaji na wananchi wanauzunguka hiyo ranchi ila ni hao wahuni kutumia vibaya fedha za ujenzi na kuacha ujenzi katika hiyo hali ya kusikitisha. Nilitegemea wahusika wote kuwa wameshakamatwa na wapo wanaozea magerezani lakini bado tu waziri anaendeleza maneno na maonyo ambayo kwa muda huu hauhitajiki zaidi ya "action". ACTION SPEAK THAN WORDS. Kila mradi ukiiba billion 5.7 tutakuwa tunaenda mbele au tunarudi nyuma??? NI KIASI GANI KINAIBIWA KAMA MRADI MMOJA TU WATU WANAIBA KIASI HICHO????
ReplyDeleteThere is a time when the government will sack everybody - the country has been rotten for a long time and It is very very hard to clean it by timua timua. Lock them up.
ReplyDeleteMake them political detainees then courts will not free them.
How about the previous Ministers who were responsible in overseeing all that shit. They should be accountable!!
ReplyDeleteHawa nivifaranga tu, majogoo watoto wao wanaishi ulaya etc etc
Hongeraa mheshimiwa kwa kazi yako, lkn nauliza hivi, hizo Fedha ziloliwa jee? Na Hao walokula hizo fedha watachukuliwa hatua gani ili kurudisha? Maana ushaagizwa zifanywe hesabu za kutolewa nyengine
ReplyDelete