Chumba cha habari cha GLOBU ya Jamii kimepata taarifa kuwa Basi la abiria  la kampuni ya Luwinzo (ambalo namba zake za usajili hazijafahimika mapema),lifanyalo safari zake Dar-Njombe inaelezwa kuwa limepata ajali asubuhi hii likitokea Njombe kuelekea Dar kwa kuligonga Lori (ambalo nalo namba zake za usajili hazikufahamika mapema), kwa taarifa za awali ambazo bado hazithibitishwa na jeshi la Polisi zinaeleza kuwa kuna vifo vya watu kadhaa,ambayo idadi yake haijajulikana mpaka sasa sambamba na majeruhi.

TUTAZIDI KUPEANA TAARIFA ZAIDI KADIRI YA ZITAKAVYOKUWA ZIKIPATIKANA.
 Baadhi ya Abiri na Wasamalia wema wakisaidia kuwaokoa baadhi ya abria waliokuwa wamenasa ndani ya basi hilo.
 Baadhi ya abiria wakiwa kwenye masikitiko makubwa.
 Kazi ya kuokoa baadhi ya abiria ikiendelea  
Namna basi hilo lilivyogonga Lori kwa nyuma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. jamani hii sasa imetosha. Labda JPM awaite wamiliki wa mabasi Ikulu na kutoa onyo juu ya uvunjaji wa sheria za barabarani ili waache huo mchezo wa kuleta vifo. Inauma sana jamani. Blackmpingo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...