Chumba cha habari cha GLOBU ya Jamii kimepata taarifa kuwa Basi la abiria la kampuni ya Luwinzo (ambalo namba zake za usajili hazijafahimika mapema),lifanyalo safari zake Dar-Njombe inaelezwa kuwa limepata ajali asubuhi hii likitokea Njombe kuelekea Dar kwa kuligonga Lori (ambalo nalo namba zake za usajili hazikufahamika mapema), kwa taarifa za awali ambazo bado hazithibitishwa na jeshi la Polisi zinaeleza kuwa kuna vifo vya watu kadhaa,ambayo idadi yake haijajulikana mpaka sasa sambamba na majeruhi.
TUTAZIDI KUPEANA TAARIFA ZAIDI KADIRI YA ZITAKAVYOKUWA ZIKIPATIKANA.
Baadhi ya Abiri na Wasamalia wema wakisaidia kuwaokoa baadhi ya abria waliokuwa wamenasa ndani ya basi hilo.
Kazi ya kuokoa baadhi ya abiria ikiendelea
Namna basi hilo lilivyogonga Lori kwa nyuma.
jamani hii sasa imetosha. Labda JPM awaite wamiliki wa mabasi Ikulu na kutoa onyo juu ya uvunjaji wa sheria za barabarani ili waache huo mchezo wa kuleta vifo. Inauma sana jamani. Blackmpingo
ReplyDelete