Programu ya kitaifa ya kupanda na kutunza mazingira inaanza mwezi huu, Waziri wa Maliasili na Utalii,Profesa Jumanne Maghembe, ametangaza Jijini Dar es Salaam jana.
Akizungumza katika kikao cha pamoja na Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Mungano, Bw. January Makamba, Waziri Maghembe alieleza kuwa Tanzania imetenga maeneo makubwa ya hifadhi ya misitu na mazingira ili kuhifadhi na kuongeza kuwango cha maji nchini.
Profesa Maghembe ambaye katika serikali iliyopita alikuwa waziri wa maji, alieleza umuhimu wa miti na misitu katika kuhifadhi maji na umuhimu wa maji kwa viumbe hai.
Maji katika uasilia wake huvifikishia viumbe hai vyote madini na ili kupata afya na ustawi kwa njia kupitia viiini au seli.
Kwa hiyo, alisema waziri, “maeneo makubwa haya ya hifadhi ya misitu na mazingira yametengwa ili yasaidie kupata hewa nzuri kwa afya yetu, maji, mvua, kuzuia joto kupanda na kupambana na mabiliko ya nchi kugeuka jangwa.”
Amesema kumekuwa ukataji mkubwa wa miti na uharibifu wa mazingira nchini na kueleza kwamba programu hii inalenga kuwa na mazingira bora (ecosystem), upandaji miti na utunzaji wake.
Waziri amesema kiako cha cha mawaziri husika cha kuweka mkakati wa ya kutekeleza kampeni hiyo ya upandaji miti na utunzazi mazingira cha siku mbili kitaanza tarehe 16 January na wataalam wa wizara mbili husika tayari wameagiza kuandaa kwa pamoja mkakati utakaotumika kutekeleza programu hiyo.
Mkutano wa pamoja utazingatia masuala yote ya upatikanaji wa rasirimali zitokanazo na faida ya misitu na mazingira.
Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano,Bw. January Makamba alisema suala la mazingira linagusa shughuli za wizara zote na taasisi nyingi na sekta binafsi na kueleza kuwa kuna kila sababu ya vyombo mbali mbali kushirikiana.
Amesema programu hii ya kitaifa ni ya aina yake nchini na katika utaratibu huu TAMISEMI itawashirikisha wananchi ili kila mwananchi ajivumie kupanda miti katika eneo lake.
Waziri Makamba amesema kuwa matarajio ya wazira hizi ni kwamba kwa kutumia progamu hii baada ya miaka mitano matokeo yake juu ya uhifadhi wa mazingira na misitu yawe yanaonekana yenyewe pasipo kusemewa na kutetewa na mtu yeyote.
“Tukitekeleza programu hii kwa uangalifu na kufanikiwa matunda yake yatavutia watu wote wa ndani na nje ya nchi kwa faiada ya taifa letu,” alisema Waziri Makamba.
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Mungano, Bw. January Makamba (kulia) akifafanua jambo wakati alipokutana na Waziri wa Maliasili na Utalii,Profesa Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto) makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii jinini Dar es Salaam. (Pili kushoto) ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt.Adelhelm Meru, na kulia ni Naibu Katibu Mkuu,Bw. Selestine Gesimba
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...