Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Mazingira (NEMC), Mhandisi George Pangawe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Zoezi la bomoa bomoa linaliendelea katika kingo za mto Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa usimamizi na udhibiti wa uendelezaji miji Wizara ya Ardhi na maendeleo ya Makazi, George Pangawe jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.

Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
SERIKALI yawahimiza wananchi waliojenga makazi kwenye sehemu hatarishi, kingo za mito na maeneo ya wazi kuhama kwa hiyari yao ili kupisha Oparesheni ya bomoa bomoa kuendelea bila kikwazo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa usimamizi na udhibiti wa uendelezaji miji Wizara ya Ardhi na maendeleo ya Makazi, George Pangawe wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Pangawe amesema kuwa Serikali itahakikisha haki inatendeka kwa wananchi wote pia itahakikisha haki na usawa wa pande zote wakati wa utekelezaji wa zoezi la bomoabomoa linaloendelea tangu lilipoaza tena Januari 5 mwaka huu.

Zoezi la bomoabomoa linaendelea jijini Dar es Salaam katika kingo za mto Msimbazi ili kuepusha wananchi kupatwa na madhara mbalimbali ambayo huwa yanakitokeza wakati wa mvua kubwa na masika.

Pangawe pia amesema kuwa bonde la mto msimbazi liliainishwa kama ni sehemu hatarishi kwa makazi ya binadamu tangu 1979 na wananchi wa maeneo ya mto huo wakaanza kuvamia kutokana uhaba wa maeneo ya makazi na kuanza kujenga katika kingo za mto huo.


Pia amewasihi wananchi kutii sheria za ardhi bila shuruti ili kuepukana na madhara mbalimbali yanayojitokeza pamoja na upotevu wa mali zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ni jambo la kushangaza kuona baadhi ya waandishi wanashindwa kutumia vyombo vyao kuwaelimisha wananchi juu ya ukweli wa kubomolewa nyumba zao. Madharani gazeti moja leo limeandika "Ni ukatili". Kichwa hiki ni cha kisiasa kuliko ukweli. Nawasihi waandishi wasaidie kuwaelimisha watu sheria za nchi na maeneo hatarishi. Wasiwape kiburi cha kuendelea kuvunja sheria za nchi ambazo matokeo yake ni kupoteza mali na maisha wakati wa mvua kubwa. Tujenge taifa imara linalozingatia sheria.

    ReplyDelete
  2. KAMA ENEO LA MTO MSIMBAZI LIMEJULIKANA KAMA ENEO HATARISHI TANGU 1979, VIPI WANANCHI WAMEACHIWA KUJENGA? NA KAMA SIRIKALI IMEWAVUMILIA KWA MIAKA 37, VIPI LEO KASI IMEKUWA YA AJABU HADI WATU WATUPWE NJE? NI WAZI ZOWEZI LINGEWEZA KURATIBIWA KWA UBORA ZAIDI. HAIKUBALIKI KUONA WATANZANIA PAMOJA NA WATOTO WAO WANALIA KWA KUVUNJIWA NYUMBA ZAO NA SIRIKALI YA WATANZANIA. NARUDIA UMAKINI UNAHITAJIKA MNAPOGUSA MAISHA YA WATU.
    AFTER ALL YOU ARE DOING ALL THAT FOR THE BENEFIT OF THE PEOPLE. SO DO NOT CAUSE PAIN WHEN HELPING SOMEONE, EXHAUST ALL OPTIONS WHEN DEALING WITH HUMAN LIVES. YOU HAD 37 YEAR, WHAT IS WRONG USING THE WHOLE YEAR TO ENSURE THE EXERCISE IS CONDUCTED PROPERLY.
    REMEMBER YOU ARE WORKING ON THEIR BEHALF. DO NOT ACT AS IF YOU ARE HOOLIGANS.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...