Mamlaka ya Mapato ya
Tanzania (TRA) imesema imeongeza muda kwa usajili wa vyombo vya usafiri vya Pikipiki za
magurudumu mawili na matatu mpaka Februari Mosi mwaka 2016.
Hayo yamesemwa leo na
Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Alphayo Kidata alipokuwa akizungumza na
waandishi wa Habari katika kikao chake cha kutoa taarifa kwa umma juu ya
ukusanyaji wa kodi, Kaimu Kamishna Mkuu amesema wameamua kuongeza muda wa zoezi
la usajili wa pikipiki ili kuiwapa nafasi wale ambao bado hawajasajili. “ Natoa wito kwa
wamiliki wa vyombo vya pikipiki kusajili vyombo vyao mapema ili wasipatwe na
adha itakayojitokeza baada ya muda uliotolewa kumalizika ” Alisema Kaimu
Kamishna Kidata.
Ameongeza kuwa zoezi
hilo lilikumbwa na changamoto kadhaa zilizowalazimu kuongeza muda mara mbili, ambazo
ni umbali wa vituo vya usajili na makazi ya wamiliki wa pikipiki hasa mikoani,pamoja
na upotevu wa nyaraka za kununulia pikipiki.
Aidha Kaimu Kamishna
Alphayo Kidata ameomba wananchi kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano na Mamlaka ili kutimiza azimio la Serikali ya Awamu ya
Tano ya kulijenga taifa kwa kufanya kazi na hasa kulipa kodi stahiki zinazoleta
mapato yanayowezesha maendeleo katika taifa letu.
Zoezi la usajili wa
pikipiki lilianzishwa kwa lengo la kurahisisha ukusanyaji wa mapato kutoka katika
vyombo hivyo, zoezi hili lilipangwa kukamilika tangu Desemba 31 2015 lakini
ikaonekana wengi hawakusajili pikipiki zao hivyo basi Mamlaka imetoa mwezi
mmoja mpaka Februari Mosi 2016 kwa wenye Pikipiki kusajili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...