Kazi za usafi wa mazingira kwenye maeneo tofauti Nchini katika kuanza rasmi kwa maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeonekana kuitikiwa vyema na Wananchi walio wengi pamoja na vikosi vya ulinzi hapa Nchini. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alijumuika na Wananchi hao kwa kazi za usafishaji wa Mtaro wa maji machafu unaokusanya maji kutokea mitaa ya Muembe Njugu, Kwahani, Kariakoo, Kilimani na Kumalizikia Pwani ya Kilimani. 
Akimuelezea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhandisi wa Baraza la Manispaa Zanzibar Nd. Mzee Khamis alisema Baraza la Manispaa limeanzisha mradi maalum wa usafi wa mazingira katika Manispaa ya Zanzibar kwa kuwashirikisha moja kwa Wananchi kwenye Mitaa yao. Mhandisi Mzee alisema hatua hiyo itatoa fursa pana kwa kila mwananchi kuona kwamba suala la usafi wa mazingira ambalo linapaswa kuwa la kudumu linaigusa Jamii moja kwa moja badala ya kufikiria kuwa jukumu hilo ni la Baraza la Manispaa pekee. 
Akizungumza na washiriki wa zoezi hilo la usafi wa mazingira kwa ajili ya kuanza kwa shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia Miaka 52 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwapongeza Wananchi pamoja na Vikosi vya ulinzi kwa ushiriki wao wa usafi wa mazingira. 
Katika kazi hiyo ya usafi wa mazingira kuanza rasmi kwa maadhimisho ya sherehe za kutimia Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikabidhi zawadi ya vifaa tofauti vya usafi wa mazingira kwa Kikundi cha usafi wa Mazingira cha Kilimani City. 
Vifaa hivyo vyenye Thamani ya Shilingi Laki Saba vimetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Idara yake ya Mazingira ikiwa ni muendelezo wa utaratibu iliyojipangia wa kutoa zawadi za vifaa kila mwaka kwa Vikundi vilivyoonyesha juhudi katika kushiriki kwenye usafi wa mazingira maeneo mbali mbali Nchini.
 Watendaji wa Baraza la Manispaa Zanzibar wakijumuika pamoja na Wananchi na Vikosi vya Ulinzi kwenye usafishaji wa mazingira hapo Mtaa wa Kwahani Uwanja wa Farasi Mjini Zanzibar.
 Balozi Seif akimkabidhi vifaa vya usafi wa mazingira Mwenyekiti wa Kikundi cha Usafi wa Mazingira cha Kilimani { Kilimani City } Nd. Khamis Shaali Chum  { mwenye T. Shirt Nyeupe  }vilivyotolewa zawadi na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Idara ya Mazingira.Kushoto ya Mwenyekiti huyo wa Kilimani City ni Mkurugenzi Maingira Nd. Juma Bakari Alawi na wa kwanza kutoka Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mazingira Zanzibar Nd. Juma Mjaja.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akishiriki na Wananchi, Vikundi ya vya usafi wa mazingira pamoja na Vikosi vya Ulinzi kwenye usafi wa mazingira hapo Kwahani Uwanja wa Farasi ikiwa ni kuanza rasmi kwa maadhimisho ya sherehe za kutimia Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Baadhi ya wapiganaji wa Vikosi vya ulinzi wakishiriki zoezi la usafi wa mazingira katika Mtaa wa Kwahani Uwanja wa Farasi kuanza kwa shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia Miaka 52. Picha na – OMPR – ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...