WAZIRI MKUU Mhe Kassim Majaliwa   anatarajia kuanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Ruvuma, ambapo atawasili mkoani  hapo  leo saa tisa alasiri.

Baada ya Waziri Mkuu kuwasili Uwanja wa Ndege wa Songea, atapokelewa na viongozi wa Chama na Serikali, pia atakwenda Ikulu kupokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Ruvuma.

Aidha, siku ya Jumatatu  atakuwa na shughuli za kufungua  tawi la Benki ya Posta mjini Songea, kukagua  maghala ya Wakala wa Taifa wa  Hifadhi ya chakula  (NFRA) kanda ya Songea na kukagua  makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea.

Siku inayofuata atatembelea na kukagua Hospitali ya Rufaa ya mkoa, na baadaye kuzungumza na watumishi wa hospitali  hiyo.

Siku ya nne ya ziara yaani jumatano, Waziri Mkuu atafanya majumuisho ya ziara mkoani humo, kabla ya kuagana na viongozi wa Chama na Serikali na kurejea Dar es Salaam. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...