Shule ya Sekondari ya St. Jude ya jijini Arusha kwa namna ya pekee wameelewa azma na malengo ya Shule Direct. Hawakuwahi kuwaambia Shule Direct kwa maneno lakini takwimu zinaelezea ukweli huu. 
Ni shule inayoongoza kwa kuwa na wanafunzi wengi wanaojifunza kupitia tovuti ya Shule Direct kuliko Shule nyingine yoyote; na kufuatiwa na Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Azania na ya tatu ni Shule ya Sekondari ya Kibasila. 
Wanafunzi wa shule hizi wametumia muda mwingi zaidi kujifunza kupitia Shule Direct kuliko watumiaji wengine. 
Shule hizi ni mfano wa kuigwa kwa sababu maarifa hayana mipaka, kadri tunavyojenga hulka ya kutafuta na kujifunza kwa kutumia fursa mbali mbali, hivyo ndivyo wanafunzi watakavyokuwa hata pale watakapokuwa wamemaliza shule. 
Kwa namna ya pekee, Shule Direct wanawapongeza na kuwasifu shule ya St. Jude kwa sababu wamekuwa mfano wa kuigwa. 
Shule Direct ni taasisi inayoboresha fursa za mwanafunzi kuweza kusoma, kufanya mazoezi na kujadiliana katika masomo mbalimbali na wanafunzi wenzake pamoja na walimu kwa kutumia Teknolojia. 
Elimu bora ni haki ya kila mtoto na kila mwanafunzi. Ukuaji wa Teknolojia Tanzania na barani Afrika kwa ujumla unapaswa kuwa nyenzo ya kuboresha upatikanaji wa maarifa na elimu ambapo kuna changamoto nyingi zinazowazuia wanafunzi kuipata. 
Shule Direct inaamini kwamba elimu inapaswa kupatikana saa yoyote na mahali popote kwa sababu elimu ni chachu ya kubaini uwezo na vipaji vilivyomo ndani ya mtu.
 Wanafunzi walioongoza kujifunza kupitia Shule Direct kutoka Shule ya St. Jude, (kwa kutumia majina yao ya kujisajili, wala si majina yao kwa kweli), ni iBOY, Brightstar, Nasmar, Mkavi, Chrisspros, Mathew.bob, Muller, Amaur, Shabbb, Jariss.j.jr. Tunawazawadia wanafunzi hawa “digital coins” za Shule Direct zitakazowawezesha kununua vitabu na vifaa mbalimbali kupitia hapo hapo kwenye tovuti.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...