Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
TAKWIMU za Ugonjwa wa Kipindupindu zinaonesha kupanda kwa mikoa ya Mwanza na Arusha kwa kuwa na wagonjwa 171, kutoka wagonjwa wa mwanzo 105.
Katika mkoani Arusha maambukizi yameongezeka kutoka wagonjwa 60 hadi kufikia wangonjwa 111 huku mkoa wa Mwanza maambukizi mapya kutoka wagonjwa 45 hadi 60.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalla amesema kasi ya maambukizi ya ugonjwa kwa wiki iliyopita imepungua katika mikoa ya Mbeya na Tanga huku mikoa ya Dar es Salaam na Lindi ikiwa haina taarifa za maambukizi mapya ya wagonjwa wa kipindupindu.
Kigwangalla amesema kuwa katika mikoa ambayo haijakuwa na taarifa za wagonjwa wapya wa kipindupindu wizara imetaka wadau wa mikoa hiyo kuendelea kwa jitihada walizozifanya katika kudhibiti ugonjwa huo.
Kigwangala amesema ugonjwa wa kipindupindu tangu kuanza kulipotiwa hapa nchini watu 202 wamefariki dunia.
Aidha amewataka madiwani na viongozi wa kisiasa kuhamasisha usafi wa mazingira na kushindwa kufanya hivyo wanahatarisha nafasi zao.
WAKATI HUOHUO.
Na Magret Kinabo wa Maelezo anaripoti.
WAKATI HUOHUO.
Na Magret Kinabo wa Maelezo anaripoti.
SERIKALI imezitaka kila halimashauri nchini kuhakikisha kuwa inatenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya damu ili kuwezesha wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo kuipata na kuepusha kupoteza maisha ya watu hususan wakina mamawajazwazito na watu waliathirika na ajali.
Aidha Serikali imesema damu hutolewa bure, hivyo mtu yoyote atakayeuziwa damu ataoe taarifa kwa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya au wizarani ili wahusika waeze kuchukuliwa hatua. Hivyo Watanzania wasikubali kutoa rushwa kwa ajili ya kupata damu.
Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangala katika ziara aliyoifanya leo katika Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu zilizopo jijini Dares Salaam.
Awali akitembelea ofisi hizo, Dkt Kingwangala alielezwa na Dkt . Avelina Mgasa kwamba changamoto zilizopo katika upatikanaji wa damu nchini ni halimshauri kutenga bajeti za kutosha kwa ajili ya huduma hiyo.
“ Mganga Mkuu au Mkurugenzi ambaye hatawajibika kuhakikisha damu inakuwepo katika vituo vya kutolea huduma ataripotiwa kwa mamlaka zilizomteua ili ziweze kumchukulia hatua,” alisema Dkt. Kingwangala.
Dkt. Kingwangala aliitaka mifumo ya bima nchini kuhakikisha iligharamia mifuko ya kuhifadhi damu na reagent(vitenganishi) kwa wagonjwa waowalipia huduma za afya ili kuweza kusiadi changamoto inayoikabili ofisi hiyo.
Aidha Dkt. Kingwangala aliitaka ofisi hiyo kuwa na mfumo wa kieletroniki wa kuwatambua watu wanaochangia damu, kutoa taarifa jinsi damu zao zilivyookoa miasha ya wagonjwa na kuwapa motisha ili waweze kuwa wachangiaji endelevu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...