WANAFUNZI 538 wa chuo cha Kodi ambacho ni sehemu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wametunukiwa vyeti vyao leo katika mahafali ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Pia wahitimu hao wameaswa kuwa waadilifu katika kazi zao kwani taaluma yao ni ukusanyaji wa mapato ya sehemu zao za kazi.
Wameaswa hayo na Naibu waziri wa Fedha na Mipamgo, Ashatu Kijaji wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa mahafali ya nane ya chuo cha Kodi ambacho ni sehemu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere.
amesema kuwa wahitimu wa chuo hicho wafanye kazi kwa weredi na uaminifu kwani wasipofanya hiyo hawataweza kufanya kazi hayo vile inavyopaswa.
Chuo cha Kodi ambacho ni sehemu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kitajengwa kingine huko kibaha mkoani pwani ili kuongeza wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri kwani chuo kilichopo Mwenge kimezungukwa na viwanda.
Chuo cha Kodi ambacho ni sehemu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kitajengwa kingine huko kibaha mkoani pwani ili kuongeza wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri kwani chuo kilichopo Mwenge kimezungukwa na viwanda.
Naibu waziri wa Fedha na Mipamgo, Ashatu Kijaji akizumgumza na wahitimu wa chuo cha Mamlaka ya mapato Tanzania TRA leo katika mahafari ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere leo jijini Dar es Salaam
Makamu Mkuu wa Chuo, Lewis Ishemoi akiwaita majina wanafunzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo katika mahafari ya nane ya chuo hicho ikiwa wahitimu 538 wamehitimu mafunzo yao katika chuo hicho jijini Dar es Salaam leo.
Wahitimu wakivaa kofia zao mara baada ya kutunukiwa katika mahafari yaliyofanika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.

Wahadhiri wakiwitunukiwa vyeti pamoja na zawadi mbalimbali katika mahafari ya nane ya chuo cha mamlaka ya mapato (TRA) leo jijini Dar es Salaam. kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Alphayo Kidata na Makamu Mkuu wa Chuo, Lewis Ishemoi.
Wahitimu wa Mahafari ya nane ya chuo cha Mamlaka ya Mapato (TRA) leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...