Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST), Dk. Gozibert Kamugisha, akizungumza wakati wa kukabidhiwa kwa scholarship kwa wanafunzi Edwin Luguku na John Thomas wa Shule ya Sekondari Mzumbe ambao walikuwa washindi wa jumla katika maonesho ya sayansi 2015. Wanafunzi hao walipewa scholarship hizo la taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation ya jijini Dar es Salaam. 
 Mzee Karimjee, Mwenyekiti wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
 Wanafunzi John Method (kushoto) na Edwin Luguku (wa pili kulia) kutoka Shule ya Sekondari Mzumbe mkoani Morogoro wakipokea hati zao za ufadhili kutoka kwa Karimjee na Ofisa Ubalozi wa Ireland nchini, Bi. Carlo. Wanafunzi hao waliibuka washindi wa jumla katika maonesho ya Sayansi kwa Shule za Sekondari mwaka 2015 yanayoandaliwa na taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST).


TAASISI ya Karimjee Jivanjee Foundation ya jijini Dar es Salaam leo hii imekabidhi scholarship kwa wanafunzi wawili wa Shule ya Sekondari Mzumbe, Morogoro, ambao waliibuka washindi wa jumla katika Maonesho ya Tano ya Sayansi ya YST kwa Shule za Sekondari Tanzania Agosti 2015.

Wanafunzi hao, Edwin Luguku na John Method, ambao leo hii wanakwenda jijini Dublin, Ireland kuhudhuria Maonesho ya 53 ya Sayansi, waliibuka washindi kutokana na utafiti wao wa sayansi usemao “Madhara ya Matumizi ya Mifuko ya Plastiki Tanzania na Namna ya Kupunguza Matumizi hayo” (The Effects of Using Plastic Bags in Tanzania and How to Reduce the Same).

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA. NA KUSOMA ZAIDI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...