Timu ya wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Wizara ya kilimo, mifugo na Uvuvi ,Wizara ya maji, na Umwagiliaji , Shirika l Umeme Tanzania (Tanesco) pamoja na Watalamu wa bonde la Mto Rufiji wametembelea vyanzo vya maji vinavyotiririsha maji katika mito inayomwaga maji kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji ikiwemo Mtera, Kihansi na Kidatu ili kuunganisha nguvu ya pamoja na kurejesha vyanzo hivyo katika hali yake ya awali kutokana na kuathiriwa na shughuli za kibinadamu na hivyo kusababisha kukauka na upungufu wa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.
Muonekano wa Bwawa la Kihansi kwa sasa ambalo pia
limepunguza uzalishaji wa umeme wa maji kutokana na kupungua kwa kina cha maji.
Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Wizara ya
kilimo, mifugo na uvuvi ,Wizara ya maji, na umwagiliaji , Shirika l Umeme
Tanzania (Tanesco )pamoja na Watalamu wa bonde la mto Rufiji waliotembelea vyanzo vya maji vinavyotiririsha maji katika Mabwawa ya kuzalisha umeme.
Moja ya sehemu ya mashine ama mtambo inayotumika kuzalisha
umeme wa maji katika vituo vya Kihansi, Kitadu na Mtera.
Mashine inayotumika kuondoa
taka kama vile magogo na nyingine
zanamna hiyo katika mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji.
Baadhi ya wajumbe wa Timu ya kutoka Wizara ya Nishati na
Madini,Wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi ,Wizara ya maji, na umwagiliaji ,
Shirika l Umeme Tanzania (Tanesco )pamoja na Watalamu wa bonde la mto Rufiji
wakipata maelezo ya namna ambavyo umeme wa maji huzalishwa katika kituo cha
Kihansi .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...