WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa anatarajia kuanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani
Ruvuma, ambapo atawasili mkoani hapo leo saa tisa alasiri.
Baada
ya Waziri Mkuu kuwasili Uwanja wa Ndege wa Songea, atapokelewa na viongozi wa
Chama na Serikali, pia atakwenda Ikulu kupokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa
Ruvuma.
Aidha,
siku ya jumatatu atakuwa na shughuli za
kufungua tawi la Benki ya Posta mjini
Songea, kukagua maghala ya Wakala wa
Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) kanda ya Songea na kukagua makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya
Songea.
Siku
inafuata atatembelea na kukagua Hospitali ya Rufaa ya mkoa, na baadaye
kuzungumza na watumishi wa hospitali
hiyo.
Siku
ya nne ya ziara yaani jumatano, Waziri Mkuu atafanya majumuisho ya ziara mkoani
humo, kabla ya kuagana na viongozi wa Chama na Serikali na kurejea Dar es
Salaam.
IMETOLEWA
NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMAPILI, JANUARI 3, 2016.
Ama kweli Hapa kazi tu.. kila laheri mheshmiwa
ReplyDeleteseynation.blogspot.com