JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA
RAIS
Anuani ya Simu: “TAMISEMI”
Simu Na: (026) 2322848, 2321607
2322853,
2322420
Nukushi: (026) 2322116, 2322146
2321013
Barua pepe: ps@poralg.go.tz
|
Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa,
S.L.P. 1923,
DODOMA.
|
TAARIFA KWA UMMA.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.
George Simbachawene (Mb) amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala
kumsimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Ilala Bw. Dennis. N. Mrema kuanzia leo tarehe
07 Januari, 2016 kwa kosa la kusababisha upotevu wa Mapato ya Serikali kutokana
na urasimu wa kukusudia, mazingira ya rushwa na uzembe katika utoaji wa leseni
za Biashara.
Kutokana na hali hiyo Mhe. Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais TAMISEMI ameelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Ilala kumuondoa kwenye nafasi yake Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Ilala na
nafasi yake kukaimiwa na mtu mwingine ili kupisha uchunguzi zaidi juu ya tuhuma
zilizotolewa dhidi yake.
Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI
amefikia uamuzi huu baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa
Wafanyabiashara ambao wamemlalamikia Mtendaji huyu kwa ukiukwaji wa Sheria,
Kanuni na Taratibu za utoaji wa Leseni za Biashara, Urasimu na Mazingira ya
rushwa.
Katika uchunguzi wa awali uliofanyika
kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Ilala mambo yafuatayo yamegundulika:
(i)
Ukiukwaji
wa Makusudi wa Sheria, Kanuni na Taratibu za utoaji wa Leseni za Biashara.
(ii)
Kutoa Leseni za Biashara zaidi ya 843 bila
kuwa na Vyeti vya uthibitisho wa Walipa kodi ‘Tax Clearance Certificates” hivyo kuikosesha Serikali Kodi ya
Mapato.
(iii)
Kukaa na fomu za Wafanyabiashara
336 kwa muda mrefu bila sababu za msingi.
(iv)
Kukiuka
Mwongozo wa Mkataba wa Huduma kwa wateja ambao unamtaka Afisa Biashara kutoa
Leseni za Biashara ndani ya siku 2 hadi 3 baada ya muombaji kuwasilisha maombi
yake ya kupatiwa Leseni ya Biashara.
Aidha,
Mheshimiwa Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais-TAMISEMI amewaagiza Maafisa Biashara
wote nchini watoe huduma za Leseni kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu , kuacha
urasimu na kujiepusha na vitendo vya rushwa.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais-TAMISEMI,
07 Januari, 2016.
Hizi publicity hazina maaana kabisa; Sawa mtu amefukuzwa kazi ila habari hizi kwenye media za nini?? Mbona mataifa mengine watu ufukuzwa kazi bila ya kuhusishwa media au unataka kusema viongozi wa Kitanzania hawawezi kufanya kazi bila ya media????!!
ReplyDelete2: Pili; Ningeomba kabla ya kufukuzisha watu kazi maamuzi yangewahusisha wanasheria wa Serikali ili kuona kisheria ipo sawa kumfukuza mtu kutokana na makosa husika?? Maana hatutaki kuja kupoteza pesa kama fidia kwa fukuza fukuza zinazoendelea nchini; Sheria zifuatwe kikamilifu na maamuzi yote yafuate Sheria na Katiba ya nchi.
Mwisho; Napenda kutoa pongezi kwa Mh Rais Magufuli kwa uongozi wake imara mpaka sasa na aendelee hivyo hivyo ktk kuliweka Taifa la Tanzania na watu wake ktk mazingira yenye ubora na kulifanya Taifa kuwa imara na nguvu hapa duniani.
Asante
Kutoa taarifa kwamba mhusika fulani amefukuzwa kazi ni sawa. Lakini kutoa taarifa za mhusika kusimamishwa kazi ili uchunguzi ufanyike inaweza kuwa siyo sahihi. Mara nyingi wahusika wanapokutikana hawana makosa jamii huwa imeshawahukumu na kuwahisi vibaya.
ReplyDelete