Katika ziara hiyo Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Charles Kitwanga amelisisitizia Jeshi hilo kuimarisha ukaguzi katika majengo marefu na mafupi ikiwemo vyombo vya usafiri na usafirishaji. Pia Mhe. Waziri amesisitiza kusimamia sheria ya maokozi inayowataka wananchi kupisha magari ya Zimamoto pamoja na gari la wagonjwa pindi yanapokuwa katika dharura.
“Hivi hamjui hata msafara wa Rais unalazimika kupisha gari la Zimamoto au wagonjwa? Iweje leo wananchi wasipishe magari hayo? Simamieni sheria hii” Alisisitiza Mhe. Waziri.
Aidha Mhe. Waziri aliahidi kushughulikia changamoto zote zinazolikabili Jeshi hilo changamoto hizo ni ukosefu wa vifaa, ufinyu wa bajeti pamoja na idadi ndogo ya Askari.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Charles
Kitwanga akipewa maelezo kutoka kwa Kamishna Jenerali Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji Eng; Pius Nyambacha jinsi ya upokeaji taarifa za matukio katika chumba
cha mawasiliano tarehe 08/01/2016.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Charles
Kitwanga atembelea Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na kukagua mitambo ya kuzimia
moto pamoja na maokozi, kulia ni Eng; Pius Nyambacha Kamishna Jenerali Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji tarehe 08/01/2016.
Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi Mhe. Charles Kitwanga akipewa maelezo kutoka kwa Sajini
Christopher Marwa jinsi ya kutumia vifaa vya maokozi katika gari maalumu la
maokozi alipofanya ziara katika Jeshi hilo tarehe 08/01/2016. (Picha na Kitengo cha Habari Makao Makuu ya
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji).
Sijui watakua wamekumbuka kusema mzee wajua tatizo letu kubwa maji, hua yanatuishia kabla hata hatujafika eneo la tukio hali inayopelekea wananchi kuzima moto kwa kutumia ndoo na sisi kupigwa mawe.
ReplyDelete