Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Mbogo Futakamba akitoa zawadi kwa
mfanyakazi bora wa mwaka 2015 toka DAWASCO wakati alipotembelea Shirika hilo mapema wiki hii.
Pamoja na mambo mengine alielekeza shirika juu ya utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Serikali ya
kuunganisha Wateja Milioni Moja ifikapo June 2016.
Picha na Everlasting Lyaro- DAWASCO.
WIZARA ya maji na umwagiliaji, imesema inaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mipango ya
usambazaji wa huduma za maji, inayofanywa na shirika la majisafi na majitaka jijini Dar es
Salaam (DAWASCO) na kutoa rai kwa watumishi wa shirika hilo kushirikiana ili kufikia malengo
ya utoaji wa huduma kwa wananchi.
Hayo yalisemwa jana na katibu mkuu wa wizara hiyo mhandisi Mbogo Futakamba, alipokuwa
akiwahutubia wafanyakazi wa DAWASCO, katika makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es
Salaam.
Mhandisi Futakamba, alisema kasi ya utoaji wa huduma bora za maji kwa wakazi wa jiji la Dar es
Salaam, imepunguza malalamiko mengi ya wananchi, na kwamba serikali imeanza kupata
matumaini makubwa na kujenga imani kwa shirika hilo kwa kufanikisha malengo makuu ya
usambazaji wa huduma hiyo kwa wananchi.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...