Kumekuwepo na habari za uongo na potofu katika mtandao wa jamii wa www.kenya-today.com kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atazuru Kenya kuhudhuria kumbukumbu ya marehemu Mhe. Jaramongi Odinga na Fidel Odinga Jumamosi hii. 
Inasikitisha kuona kwamba mwandishi wa Kenya anachukua nafasi ya Mwandishi wa habari wa Rais wa Tanzania kwa kuwa na  ratiba ya Mhe. Rais wa Tanzania kuliko waTanzania wenyewe. 
Haijulikani ni nini has nia ya mtandao huo, lakini ukweli ni kwamba ratiba hiyo ni batili na ya uongo uliotukuka. Hawa watani wetu wa jadi wana lao jambo!  Wapuuzeni. Taarifa hiyo si ya kweli.

Kuona habari hio ya uongo BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ukiona hivyo ujue Kenyatta maji ya shingo. Huu mtandao wa www.kenya-today.com ni wa uchonganishi. MSIUAMINI. Mafala sana hawa watu

    ReplyDelete
  2. Yaani JPM avunje protokali, japo ni rafikiye, amtembelee Odinga kabla ya Kenyatta. Huu ni uzushi. Hapo ujue mtandao huo una nia ya kupotosha mambo. JPM kamwe hawezi kufanya hivyo. Odinga ni UKAWA wa Kenya

    ReplyDelete
  3. sometimes silence is the best medicine. Just ignore them

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...