Baadhi ya maofisa wa Benki ya NBC wakipozi kwa picha wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam. Hii ni kampeni ya tatu ya kuwekeza kuzinduliwa na NBC na kama ilivyo katika miaka mingi kampeni zote zimekuwa za mafanikio makubwa katika suala zima la mrejesho na ufahamu wa wateja. Mwaka jana NBC ilizindua kampeni ya kuwekeza iliyopewa jina la “Weka Upewe” ambayo ilishuhudia NBC ikitoa zawadi kadhaa kwa wateja wao nchini kote.
 Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza cha benki hiyo, Andrew Massawe (kushoto), akizungumza kuhusu faida mbalimbali za mteja wa benki hiyo atakayeshiriki kampeni ya malengo ya NBC. Kulia ni Mkuu wa Huduma za Rejareja za Kibenki wa benki hiyo, Mussa Jallow.

 Mkuu wa Huduma za Rejareja za Kibenki wa benki ya NBC, Mussa Jallow (katikati), akikata utepe kuzindua rasmi kampeni ya  Malengo ya benki hiyo  jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo na kulia ni Meneja wa kampeni hiyo, Mtenya Cheya.
 Kampeni ya malengo itadumu kwa muda wa miezi mitatu kutoka Februari 4 mpaka Aprili 30 2016. Katika kipindi hicho cha miezi mitatu ya kampeni,wateja wanaoweka fedha watafaidika na  kiwango cha kuvutia cha riba na kuwa katika nafasi kubwa ya  kushinda gari mpya aina ya Toyota Land Cruiser Prado kama linavooeneka pichani.
Mkuu wa Huduma za Rejareja za Kibenki wa benki ya NBC, Mussa Jallow (kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza cha benki hiyo, Andrew Massawe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. mmmh hizi picha zilipigwa kwa simu nini? tena mchina. kitengo cha PR nunueni camera ya kisasa mpost picha zinazoeleweka acheni hizo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...