Hoyce Temu

Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akimlisha chakula Narsa Ramadhan (2) akiwa na mama yake Tatu Saleh (kushoto) wakati wa hafla ya chakula kilichondaliwa kwa watoto na wazee wanaoishi katika makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.

Na Modewjiblog)

Licha ya kuvaa taji la ulimbwende, Miss Tanzania 1999, Hoyce Anderson Temu amekuwa mfano wa kuigwa kwa walimbwende waliopita wa taji hilo nchini kwa kujitoa kusaidia jamii ya Tanzania kwa kutumia nafasi aliyonayo nchini.
Hoyce ambaye ni mzaliwa wa Arusha amekuwa mstari wa mbele kusaidia Watanzania ambao wanamatatizo mbalimbali kama ya kiafya na elimu ambapo amekuwa akitoa misaada na muda mwingine kutafuta wadhamini ili kusaidia jamii ambayo ameifikia kwa muda huo.
Baadhi ya mafanikio ambayo yamepatikana kupitia kipindi cha Mimi na Tanzania ni pamoja na kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya kupata matibabu akiwepo mtoto Hamisi ambaye alimsaidia kwenda kupata matibabu ya mguu wake.
Kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania kinachorushwa upitia Channel Ten kila siku ya jumapili, saa 9:30 usiku, Hoyce amefanikiwa kuandaa vipindi zaidi ya 1,000 maeneo mbalimbali nchini na katika maeneo yote ambayo ametembelea amefanikiwa kutoa msaada kulingana na mahitaji yanayohitajika. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. How naive? Hivi kweli Watanzania wanasaidiwa kwa kulishwa chakula mdomoni? Mobilize resources ama food stocks. That's the way u helpf; not by hand feeding! Hao mama zao can do that! Get real!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...