Rais Mstaafu wa amamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete amekutana na Makamu wa Rais wa Sudani Kusini Riek Machar akiwa mjini Addis Ababa, Ethiopia pembezoni mwa Mkutano wa Mawaziri wa Afrika kuhusu Chanjo.
Katika mazungumzo yao, Mheshimiwa Machar alimshukuru Rais Mstaafu Kikwete na Mwenyekiti wa CCM kwa mchango ambao CCM imeutoa katika kusuluhisha mgogoro ndani ya chama tawala cha SPLM uliopelekea kufikiwa kwa makubaliano ya Arusha. Ametumia pia fursa hiyo kuomba CCM kuendelea kukisaidia chama cha SPLM kutokana na uzoefu na ukomavu wake wa uongozi. Amemhakikishia Rais Mstaafu Kikwete juu ya azma yake ya kurejea Juba mapema iwezekanavyo.
Kwa upande wake, Rais Mstaafu Kikwete amempongeza kwa utayari wake wa kurejea Juba na amemuhakikishia kuwa CCM haitatupa mkono SPLM na itaendelea kushirikiana na kutoa mchango wake pale utakapohitajika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...