Leo Februari 24,2016 ,Chama cha Kimataifa kinachotoa misaada mbalimbali ya Kijamii cha Lions Club International chenye makao yake makuu nchini Marekani kimetoa msaada wa madawati 165 yenye thamani ya shilingi milioni 18 katika shule ya msingi Town na Mwenge zilizopo katika manispaa ya Shinyanga ili kumaliza changamoto ya wanafunzi kukaa chini.

Pichani viongozi wa wilaya ya Shinyanga,wazazi na maafisa kutoka Lions Club International wakiongozwa na Gavana wa Lions Club katika nchi ya Tanzania, Uganda na Sudani ya Kusini bwana Hyderali Gangji wakiwa katika shule ya msingi Town...Madawati hayo 165 yametolewa na Lions Club ya mkoa wa Mwanza.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama  Malunde ametuletea picha 30 kilichojiri mwanzo hadi mwisho.Gavana wa Lions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji alisema wamekuwa wakitoa misaada mbalimbali mkoani Shinyanga ambapo mwaka jana walitoa msaada wa chakula kwa wahanga wa mvua ya Mwakata wilayani Kahama,pia chakula katika kituo cha walemavu wa ngozi cha Buhangija,kutoa madawati katika shule ya msingi Town na Mwenge  Miongoni mwa madawati ya chuma 165 yaliyotolewa na Lions Club International katika shule ya msingi Town na Mwenge katika manispaa ya Shinyanga.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...