Na Bashir Yakub .
Masuala yanayohusu ardhi ni masuala nyeti sana. Unyeti wa masuala haya unatokana na ukweli kuwa maisha yote yamejengwa juu ya ardhi. Hakuna kilichowahi kufanywa, kinachofanywa na kitakachofanywa nje ya ardhi. Iwe kutembea, kuendesha kipando, kula, kulala, maendelezo yoyote ya teknolojia, ujenzi, maji safi na salama, kupata chakula, hata unaporuka hewani iwe kwa ndege au kifaa kinginecho huwezi kusema sijatumia ardhi kwakuwa hata mruko wenyewe(take off) huanza na ardhi.
Lakini pia hata uruke na ukae huko miaka 200 bado utatakiwa kurejea ardhini. Ardhi ni kila kitu kwa maana ya kila kitu. Kupitia msingi huu tunapata umuhimu mkubwa wa kueleza kila lililo la msingi kuhusiana na masuala ya ardhi hususan umiliki wake.
Kupitia makala hizi yalishaelezwa mengi kuhusu namna ya kununua ardhi, namna ya kuepuka migogoro wakati wa ununuzi, namna ya kubadilisha hati na mengine . Fursa ya leo itaeleza umuhimu na faida za kuwa na hati.
1.NINI MAANA YA HATIMILIKI .
Hati miliki ya ardhi hujulikana pia kama “Title Deed”. Hatimiliki ya ardhi ni nyaraka maalum inayotolewa na wizara ya ardhi ikionesha mwenye haki ya umiliki wa ardhi, eneo na kiasi anachomiliki huku ikiainisha wajibu na haki alizonazo mmiliki huyo.
Wajibu katika hatimiliki ni yale unayotakiwa kutekeleza kwa mfano malipo ya kila mwaka, matumizi yaliyopangwa, na kila sharti analotakiwa kutekeleza mmiliki.
Haki katika hatimiliki ni yale yote anayostahili kupata mmiliki wa ardhi husika ikiwemo taarifa ( notice) rasmi panapo mabadiliko yoyote katika matumizi na umiliki, haki ya fidia, na haki ya kuwa huru katika matumizi halali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...