Na Bashir Yakub.
Mara kadhaa tumeeleza namna ya kusajili kampuni. Yumkini tulipoeleza hivyo tulirejea usajili wa kampuni zilizo Tanzania. Tulieleza faida za kufanya biashara chini ya kampuni na tukaeleza namna ya kisheria ya kusajili kampuni mwanzo mpaka mwisho unapopata cheti cha kuzaliwa kwa kampuni( certificate of incorporation). Hatujawahi kueleza usajili wa kampuni ambayo imeanzishwa nje ya Tanzania inayohitaji kufanya biashara Tanzania.
1.KAMPUNI ILIYOSAJILIWA NJE YA TANZANIA.
Tunaposema kampuni kusajiliwa nje ya Tanzania tunamaanisha kampuni imeanzishwa nje ya Tanzania na cheti chake cha usajili imekipata huko nje ya Tanzania na hivyo inatambulika kama kampuni ya huko ilikosajiliwa. Kampuni ya namna hii inaweza kuamua kuja Tanzania kufanya biashara bila kuhitaji kuanzisha kampuni nyingine mpya isipokuwa kuendeleza ileile na kupafanya Tanzania kama tawi au si tawi lakini sehemu kuu ya biashara.
2. WATANZANIA WALIO NJE YA NCHI KUMILIKI MAKAMPUNI HAYA.
Baadhi ya Watanzania walio nje ya nchi wamewahi kuuliza swali hili wakitaka kujua utaratibu wa kufuata ili kuifanya kampuni iliyoanzishwa nje ya Tanzania kuweza kufanya kazi zake Tanzania.
Kwa waliouliza swali hili watapata majawabu lakini pia itafahamika kwa wengine kuwa unaweza kuunda kampuni hukohuko uliko ikafanya kazi huko lakini pia Tanzania ambako ni nyumbani kukawa na tawi la biashara .
Lakini pia wapo watu ambao huulizwa swali hili na rafiki zao wa kigeni kuhusu kuingiza kampuni Tanzania kwa ajili ya biashara. Hawa nao sasa watakuwa na majawabu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...