Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (watatu kulia) akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole (wapili kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia), Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke (wapili kulia) wakielekea katika hafla fupi iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa ajili ya kumuaga Mwakilishi wa UNHCR nchini, iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza katika hafla ya kumuaga Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole (watatu kulia). Katika hotuba yake fupi, Waziri Kitwanga alimshukuru Mwakilishi huyo kwa ushirikiano wake mzuri kati ya Wizara na UNHCR, pia alimtakia safari njema na mafanikio mema arudipo nyumbani kwake. Joyce anatarajia kustaafu rasmi katika nafasi hiyo mwezi ujao. Wanne kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni, kushoto aliyekaa ni Katibu Mkuu, Meja Jenerali Projest Rwegasira, na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole, kwa ajili ya kumbukumbu yake kutokana na ushirikiano mzuri kati ya Shirika lake la UNHCR na Wizara. Hafla hiyo fupi ya kumuaga iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ilifanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.
Diplomasia ni pamoja na uwiano. Inakuwaje mwakilishi wa shirika moja anaagwa na uongozi wote wa Wizara?!!!! Ana umuhimu gani wa kihivo? Hawa jamaa wameturubuni kuwapatia uraia warundi zaidi ya laki moja hata bila kuwasambaza maeneo mbali mbali nchini na bila kuwalipa wananchi wetu wakazi wa mipakani maeneo yao yaliyocjukuliwa na kisha anaagwa kwa kushabikiwa hivyo? Isiyoshe wakaachwa hapo hapo mpkakani karibu na wanapotoka ili waendelee kuwa chanzo kwingine cha mgogoro na Burundi miaka ya usoni! Yashangaza sana nchi yetu?
ReplyDeleteUtadhani watu wamenunuliwa ama hawaipendi nchi yao. Tizama Ulaya wanavyogombana kuchukua mkimbizi hata mmoja kutoka Syria. Sisi viongozi wetu wamelala na kujichana tu! Mungu Ibariki Tanzania