Na Bakari Issa Madjeshi

Klabu ya Soka ya Manchester City ya nchini Uingereza leo itakuwa na kibarua kigumu cha kupambana na Klabu ya Dynamo Kyiv ya nchini Ukraine katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya (UEFA CHAMPIONS LEAGUE).

Manchester City ikiwa chini ya Manuel Pellegrini itaingia katika kipute hicho ikiwa na kumbukumbu ya  kupoteza mchezo wake wa Kombe la FA dhidi ya Chelsea kwa kukubali kichapo cha mabao 5-1, siku ya Jumapili.
Hata hivyo,Kocha wa Kikosi hicho Pellegrini alitetea uamuzi wake wa kutowapanga wachezaji wake muhimu akiwa na haya yakusema ”Ilitubidi kufanya maamuzi magumu dhidi ya Chelsea lakini ndio uamuzi pekee tuliokuwa nao kwa wakati ule”

“Tulikuwa na wachezaji 13 kwa hiyo lilikuwa ni kusudi letu kuendelea katika michuano yote na hatukuweza kufanya hivyo”

“Kitu cha muhimu ni ufanisi wa wachezaji wetu muhimu. Ni dakika 90 za mwanzo za michezo miwili,chochote kitakachotokea ,sio mwisho wa mchezo wa mkondo wa kwanza”,alieleza  Pellegrini

Pia, Pellegrini atamtumia mlinzi wa kushoto, Eliaquim Mangala alierejea uwanjani baada ya kuwa majeruhi tangu Januari 6 ya mwaka huu,wakati huohuo Kocha huyo atawakosa Winga Kevin de Bruyne na Jesus Navas,viungo Samir Nasri na Fabian Delph na Mshambuliaji Wilfred Bony.
Kwa upande wa Dynamo Kyiv ambayo haikucheza mchezo wowote wa kiushindani tangu ilipokumbana na Maccabi Tel Aviv katika hatua ya makundi ya Ligi hiyo ya Mabingwa Ulaya,Desemba 9 mwaka jana.

Hata hivyo,Kocha wa Kikosi hicho cha Ukraine, Sergei Rebrov anahofu ya kumkosa winga wake machachari, Andriy Yarmolenko ambaye alikua anasumbuliwa na maumivu ya goti aliyoyapata katika mchezo dhidi ya Maccabi

Je? tuone ndani ya dakika 90 nani atacheka na nani atalia...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...