Na MatukiodaimaBlog

MBUNGE wa jimbo la Isimani Bw Wiliam Lukuvi amewapa pole waathirika wa mafuriko wa kata ya Mapogolo tarafa ya Idodi wilaya ya Iringa mkoani Iringa kwa kuwakabidhi msaada wa pesa zaidi ya Tsh milioni 9 kwa ajili ya kusaidia mahitaji mbali mbali ikiwa ni pamoja na kurejesha miundo mbinu ya maji safi iliyoharibiwa na mafuriko.

Bw Lukuvi ambae pia ni waziri wa Ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi alikabidhi msaada huo jana baada ya kutembelea waathirika hao waliopo kambi ya Kitanewa pamoja na kutembelea eneo la barabara ya kutoka Iringa  kuelekea hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambayo kwa sasa imekarabatiwa baada ya awali barabara hiyo kukatika kutokana na mafuriko hayo , alisema kuwa lengo lake kama mbunge wa jimbo hilo la Isimani na serikali ni kuona wananchi waliokumbwa na mafuriko wanaendelea kusaidiwa .
 
Mbunge wa jimbo la Isimani Bw Wiliam Lukuvi ambae ni waziri wa Ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi (kulia) akimpa maelekezo mwenyekiti wa kijiji cha Mapogolo baada ya kumkabidhi fedha kiasi cha Tsh milioni 2 za kulipa fidia ya ardhi kwa wananchi watakaohamishiwa makazi mapya kutoka kitongoji cha Kitanewa Idodi ambao nyumba zao zilisombwa na mafuriko.

Alisema kuwa awali aliomba msaada wa mahindi tani 100 kutoka serikali kwa ajili ya waathirika hao wa mafuriko Idodi na Pawaga ikiwa ni pamoja na kuwasaidia msaada wa fedha kiasi cha zaidi ya Tsh milioni 3 kwa ajili ya kuwawezesha waathirika hao wa mafuriko kupata mahitaji mengine kama mboga na pesa ya kusagia mahindi hayo .

Bw Lukuvi alisema kuwa kwa ajili ya kurejesha huduma ya maji kijijini hapo  amewasaidia kiasi cha Tsh miliobni 4 ambazo wameomba kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu hiyo ,pia kiasi cha Tsh milioni 2 kwa ajili ya kukiwezesha kijiji kulipa fidia ya ardhi kwa wananchi waliotoa ardhi yao kwa ajili ya wakazi wa kitongoji cha Kitanewa ambao wanapaswa kuhamishwa eneo hilo la mafuriko la kupewa makazi mapya . 
Wananchi wanaotakiwa kuhamishwa kwenda makazi mapya baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko wakimsikiliza kwa makini mbunge wao Lukuvi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hiyo picha ya mwanzo ingekuwa haina maelezo yeyote, nadhani kila mtu angeibuka na 'caption' yake kichwani. By the way, poleni sana wote mlioathirika na mafuriko Idodi, Mkoani Iringa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...