Na Mwandishi wetu, Iringa 
Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Iringa zimesomba mashamba na nyumba na kuwaacha wananchi wengi wakiwa hawana mahali pa kukaa. 
Vitongoji vilivyo athirika sana ni Kisanga, Nyallu, Makoka na Mbughani. Mpaka sasa bado idadi isiyo rasmi inakadiliwa watu zaidi ya 200 bado wamezingirwa na maji siku ya 4. 
Juhudi za uokoaji zikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela zimefanikiwa kuokoa watu 399 kitongoji cha Kisinga, watu 38 kutoka kitongoji cha Makoka, na watu 23 kutoka kitongoji cha Nyalu. Jeshi la polisi lilitoa helicopter kusaidia uokoaji na pia kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kilikuwa mstari wa mbele kwenye zoezi hilo. 
Maeneo mengi yalihitaji waogoleaji mahiri ili kuwafikia wananchi. Zoezi linaendelea hado sasa. shule 2 zimetengwa kwa ajili ya kupokea wahanga wa mafuriko shule ya msingi Itunundu na shule ya msingi Kisanga.
kitongoji cha Nyalu wamezingirwa na maji


Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiongoza uokoaji wa wananchi walioathirika na mafuriko kijiji cha Pawaga
Eneo lililoathirika
Njia haipitiki kwa vyombo vya moto
Familia zikiwa imezingirwa na maji.
Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera mkuu kwa kusaidia, ila mbona unavua viatu na kuacha miguu wazi wakati kazi ya viatu ni kuzuia mguu usijikate au kuumia na vitu kama vyupa,nk pia thamani ya mguu ni kubwa kuliko hivyo viatu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...