Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu ametembelea hospitali ya Taifa Muhimbili kukagua utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kuwataka watumishi wa wizara hiyo waliokuwa wakilitumia jengo la Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto kuhamisha ofisi zao na kuliacha kwa ajili ya matumizi ya wodi ya wazazi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo katika hospitali hiyo, Waziri Ummy amesema kuwa mpaka kufikia kesho tayari jengo hilo litakuwa limeanza kutumika kwa kuwa watafanya kazi ya kuhamisha makabrasha ya watumishi hao usiku kucha kuhakikisha agizo la Rais John Magufuli linatekelezwa mara moja.
FSA_6533

Picha mbalimbali zinaonesha Waziri Ummy Mwalimu akikagua utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli pamoja na watumishi na vibarua wakihamisha nyaraka na makabrasha mbalimbali kutoka kwenye jengo lililokuwa likitumiwa kama ofisi na watumishi wa wizara hiyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.

FSA_6416FSA_6443


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...