JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz              

Faksi: 255-22-2113425



OFISI YA RAIS,
      IKULU,
 1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za pole Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Tunu Pinda aliyepatwa na ajali ya gari, iliyotokea jana tarehe 08 Februai, 2016 akiwa safarini kutoka Dodoma kwenda Dar es salaam.

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Mkundi lililopo katika Manispaa ya Morogoro ambapo gari aliyokuwa akisafiria Mama Tunu Pinda, ilipinduka baada ya kumgonga mwendesha pikipiki aliyeingia ghafla barabarani.

Katika salamu hizo alizozituma kupitia kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko taarifa za kutokea kwa ajali hiyo na amemuombea Mama Pinda na Majeruhi wengine kupona haraka.

"Kupitia kwako Mheshimiwa Waziri Mkuu Pinda, naomba unifikishie pole nyingi kwa mkeo Mama Pinda kwa kuumia katika ajali hii, na namuomba Mwenyezi Mungu awaponye majeruhi wote ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku" alisema Rais Magufuli.

Mama Tunu Pinda anaendelea kupata matibabu Jijini Dar es salaam, na hali yake inaendelea vizuri.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
09 Februari, 2016

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...