Na Teresia Mhagama, Mtera
Imeelezwa kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuendeleza miradi mbalimbali ambayo wananchi wameamua kuiendeleza ikiwemo miradi ya uzalishaji umeme kwa kutumia vyanzo mbalimbali kama maji,upepo, jua, nishati jadidifu, makaa ya mawe na mawimbi ya bahari.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati wa kikao chake na wazalishaji wa umeme wa maji na wale wanaotaka kuzalisha umeme huo chini ya megawati 20 kilichofanyika katika Kituo cha Kuzalishia Umeme cha Mtera.
“Serikali lazima iwe Msemaji wa wawekezaji hawa ili kuhakikisha wanapata fedha na teknolojia za kuendesha miradi yao na hii itapelekea Taifa kuwa na nishati ya kutosha kwani wawekezaji hawa sasa watakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme,” alisema Profesa Muhongo.
Ili kufanikisha suala, Profesa Muhongo aliwataka wadau hao wanaotaka kuzalisha umeme wa maji chini ya megawati 20 kuhakikisha kuwa wanaandika na kuwasilisha wizarani mapendekezo yanayochanganua miradi wanayotaka kuanzisha kabla ya mwisho wa mwezi huu ili litengenezwe kalabrasha moja litakalotumika katika kuombea fedha kwa wafadhili mbalimbali na Taasisi za Kifedha.
“Ifikapo tarehe 28 mwezi huu mchanganuo wa mapendekezo yenu yawe yamemfikia Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Nishati ili serikali iangalie namna ya kutafuta fedha zitakazowawezehsa kuendeleza miradi yenu ya umeme badala ya mtu mmoja mmoja kuanza kuzunguka na maombi yake binafsi ya kutafuta fedha kutoka Taasisi mbalimbali jambo linalochelewesha upatikanaji wa fedha hizo, “ alisema Profesa Muhongo.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...