SHIRIKA la Ndege la Etihad na mshirika wake Jet Airways wametangaza ongezeko la asilimia 63 la wasafiri wanaoenda na kuondoka nchini India. Ongezeko hilo limeipa nguvu mpya ushirikiano huo na kuimarisha azma yake ya kuwa moja kati ya ndege zenye soko kubwa.
Kwa pamoja, mashirika haya yameweka rekodi ya kuasafirisha abiria milioni 3.3 baina ya vituo vyake vya Abu Dhabi na India mwaka 2015, kwa kulinganisaha mashirika hayo yalisafirisha abiria milioni 2 ndani ya miezi 12 iliyopita.
Etihad limekuwa shirika geni la kwanza lililowekeza katika shirika la Ndege la Kihindi chini ya Sheria ya Uwezekaji kutoka nje ya nchi ya India ambapo liliwekeza dola za Kimarekani milioni 750 katika Jet Airways ili kupata hisa asilimia 24 mwaka 2013. Shirika la Etihad leo lina ndege 175 kwenda miji 11 India kila wiki. Mitandao ya Etihad na Jet Airways kwa pamoja imewezesha safari za ndege 250 kila wiki katika ya Abu Dhabi na miji 15 ya India.
Pamoja, mashirika haya yanaongoza katika soko kwa usafiri kati ya India na UAE. Kwa kuangalia soko la kimataifa, wanasafirisha asilimia 20 ya abiria kutoka na kwenda India na hii inawakilisha hisa kubwa ya sekta usafiri wa anga nchini India.
Kwa kuongezea, Etihad inafanya operesheni ya uchukuzi mara 14 kila wiki kwenda miji 4 India na inaingiza na kutoa tani 120,000 za mizigo kila mwaka- hii inawakilisha asilimia 9 ya jumla ya soko la kimataifa.
Takwimu hizi zinaonesha umuhimu wa Shirika hili katika soko la India - moja katika ya vyanzo vikubwa vya biashara kwa Etihad- kwa ushirikiano wake mkubwa na Jet Airways na kuimarisha mahusiano kati ya UAE na India.
Mahusiano kati ya nchi hizi mbili ndio yalikuwa kiini cha mazungumzo yaliyotokea Mumbai na Delhi wiki iliyopita ambayo yalileta makubaliano mapya katika sekta mbalimbali ili kukuza mikakati na biashara za kiuchumi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...