Baraza la waislamu mkoa wa Dar es salaam launga mkono maamuzi ya tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC, kufanya marudio ya uchaguzi huku likitoa rai kwa vyama vyote vya siasa kushiriki uchaguzi huo. https://youtu.be/BSYi6AYGCKY
Harakati za ubomoaji wa jengo la ghorofa 16 lililoko jijini Dar es salaam zaanza kuonekana baada ya wajenzi kuanza kupangua mbao na vyuma viliyotumika katika ujenzi wa jengo hilo. https://youtu.be/G4iCY8D2di0
Tume ya taifa ya uchaguzi NEC yabainisha changamoto ya elimu kwa mpiga kura huku ikitoa rai kwa serikali na mashirika ya kimataifa kuweka utaratibu wa kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya kufadhili asasi za kiraia ili ziweze kutoa elimu hiyo kwa wananchi. https://youtu.be/Aiv3N70rqrs
Agizo la Rais Magufuli ya kuwataka wananchi kuweka mazingira yao safi, yaonekana kuendelea kukumbwa na changamoto kufuatia uhaba wa magari ya kuzolea taka jambo linalopelekea mrundikano wa taka katika maeneo mbalimbali ya jiji. https://youtu.be/jD7PZH5936Y
Wakati jeshi la polisi likiendelea kuwakamata waendesha pikipiki wanaoingia katikati ya jiji maarufu kama bodaboda, duru zaonyesha vijana hao kubuni mbinu mpya ya kuingia mjini licha ya kuwa hatarishi.https://youtu.be/WOn_WDJ-eT0
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam lasitisha maandamano ya baraza la vijana Chama Cha Demokrasia na Maendeleo BAVICHA;https://youtu.be/3FhRA9VQg8g
Serikali yasema bado inatafuta pesa toka nje ya nchi ili kukamilisha mradi wa umeme vijijini REA; https://youtu.be/2FagO8SknYY
Inaelezwa kuwa mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Mtwara zasababisha uharibifu wa miondombinu; https://youtu.be/A9MAttR63F0
Zaidi ya wanafunzi 5000 kutoka kaya masikini mkoani Iringa wanufaika na mradi wa TASAF wenye lengo la kuzisaidia kaya masikini kiuchumi;https://youtu.be/2XpgYq8fl-A
Kampuni ya kufua umeme ya IPTL yasema inalipwa na TANESCO kila siku kiasi cha shilingi milioni 40 hadi milioni 104 kila siku kama gharama ya kuuziana umeme baina ya TANESCO NA IPTL; https://youtu.be/OPSFEU4mltE
Kocha wa timu ya Mgambo JKT ajitamba kuitandika timu ya Simba katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara utaochezwa jumatano hii;https://youtu.be/aKKpVnJmr10
Baadhi ya wabunge waitaka serikali kuboresha usafiri wa Treni nchini kwa kuboresha miundombinu ya Reli; https://youtu.be/RPtyFpk8lbQ
Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi, Mhe. William Lukuvi apiga marufuku kwa wawekezaji wa kigeni kuuza ardhi kwa wenzao;https://youtu.be/byTxTD56kRk
Jeshi la polisi mkoani Morogoro linawashikilia raia 12 wa Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini kinyume na sheria; https://youtu.be/usf7PLOUaek
Mkuu wa wilaya ya Msoma aagiza kufukuzwa kazi kwa afisa mtendaji wa kata ya Mshikamano kwa tuhuma ya ubadhilifu wa fedha za umma;https://youtu.be/tMut5uNmKNo
Wakazi wilayani Uyui mkoani Tabora walazimikia kutumia magome ya miti kufutia daraja kusombwa na maji; https://youtu.be/x5Tqv9zUON8
Timu ya Prisons ya jijini Mbeya yajinasibu kuitandika timu ya Yanga katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara utakaochezwa jumatano ya wiki hii;https://youtu.be/uQtX3ULkha0
Mtoto mmoja nchini Afghanistan aushangaza ulimwengu baada ya kutengeneza jezi kwa kutumia mifuko ya plastiki kama sehemu ya kufikia ndoto yake ya kuwa kama Lionel Mesi; https://youtu.be/JsBGFQ-3jWo


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...