Na John Nditi, Morogoro
POLISI mkoani hapa leo imewatia mbaroni wahamiaji haramu 12 kutoka nchini Ethiopia pamoja na watanzania wawili katika eneo la Mikumi, barabara kuu ya Morogoro- Iringa.
Wahamiaji hao haramu walikamatwa usiku wa kuamkia Februari 2, mwaka huu majira ya saa nane na nusu usiku wakiwa katika gari lenye namba za usajili T 876 BHZ aina ya Toyota Noah , iliyokuwa ikiwndeshwa na Kimu Mustafa (25) mkazi wa Segera, mkoani Tanga akiwa na Kondakta wake aitwaye Rashid Ally (17) pia mkazi wa Segera Tanga.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonaerd Paulo, dereva wa gari na kondakta wake walieleza kuwa walielekezwa na tajiri wao kuwapakia wahamiaji haramu hao kutoka Mji wa Chalinze , mkoa wa Pwani.
Kamanda huyo alisema, kwa mujibu wa dereva huyo , kuwa tajiri wake alimpingia simu akiwa Segera na kumwelekeza kuwa aende Chalinze kuwachukua watu na kuwapeleka hadi Tunduma kwa vile walikuwa wakienda nchi ya Afrika Kusini.
Kamanda Paulo alisema kuwa uchunguzi wa awali umeonesha kuwa wahamiaji haramu hao walikuwa wanasafirishwa hadi Tunduma ili baadaye waelekee Afrika Kusini.
Amesema watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na kuwatafuta wafadhili wa biashara hiyo haramu na baada ya uchunguzi kukamilika watafikishwa Mahakamani.
Gari walilokuwa wakitumia wahamiaji haramu wa Ethiopia ( mbele ) waliokamatwa likiwa nje ya jengo la Kituo Kikuu cha Kati cha Polisi mjini Morogoro.
Wahamiaji haramu wa Ethiopia waliokamatwa na Polisi, jana wakiwemo na watanzania wawili ,eneo la Mikumi, wilayani Kilosa katika barabara kuu ya Mikumi- Iringa, wakiwa chini ya Ulinzi wa Polisi eneo la viwanja vya Jengo la Kituo Kikuu cha Kati cha Polisi mjini Morogoro.
Wahamiaji haramu wa Ethiopia ( mbele ) waliokamatwa wakiwasili eneo la viwanja vya Jengo la Kituo Kikuu cha Kati cha Polisi mjini Morogoro.
Wahamiaji haramu wa Ethiopia ( mbele ) waliokamatwa wakiwasili eneo la viwanja vya Jengo la Kituo Kikuu cha Kati cha Polisi mjini Morogoro.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, akielezea jambo kwa waandishi wa habari , mbele ya wahamiaji haramu wa Ethiopia waliokamatwa usiku wa kuamkia Februari 2, mwaka huu pamoja na watanzania wawili eneo la Mikumi, wilayani Kilosa katika barabara kuu ya Mikumi- Iringa, baada ya kuwapatia mji wa Chalinze na kwenda nao Tunduma ili wavuke mpaka kuelekea Afrika Kusini. Picha na John Nditi







Warudisheni tu kwao, ni njaa tu imewaleta. Mzee Magufuli anapiga mabao ya mbali kimya kimya, amakweli hapa kazi tu
ReplyDeleteLet's be reasonable. We can do this exercise at less cost. If those immigrants were going out of country at their own cost why bother. Entering should be hard not leaving. Now you have to care for them. Be reasonable
ReplyDeleteKwanza hawaelekei bongo. Wanaelekea zao South Africa. Bongo kwenyewe njaa kali nako. Wala hakuna tofauti na walikotoka. Hata huko South ni hivyo hivyo nako. Kwa hiyo wasiwanyanyase na wawape chakula ni halakati za mangaiko tu binadamu
ReplyDelete