Shirika la Maendeleo ya
Petroli Tanzania (TPDC) liliandaa semina ya waandishi wa Mkoa wa Mtwara, Semina
hiyo ililenga kuwajengea uwezo waandishi hao kuielewa sekta ya mafuta na gesi
asilia mchini.
Akifungua semina hiyo
kwaniaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Meneja wa Mawasiliano kutoka TPDC Marie
Msellemu alisema semina hiyo anaamini itawajengea uwezo waandishi hao hasa
wanapo toa taarifa za mafuta na gesi asilia kwa wananchi.
Watoa mada katika semina
hiyo kutoka TPDC walitoa mada zilizo gusa shughuli nzima za Shirika kuanzia
utafiti wa gesi asilia na mafuta hadi matumizi ya rasilimali hizo.
Kwa upande wao waandishi wa
habari walioshiriki semina hiyo wameipongeza TPDC kwa jitihada hizo za kutoa mafunzo
kwao, zaidi waandishi hao wametaka mafunzo hayo yawe endelevu kwao.
Meneja wa Mawasiliano kutoka Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Marie Msellemu akifungua semina ya
waandishi wa habari wa Mkoa wa Mtwara, semina hiyo ilifanyika Manispaa ya
Mtwara Mikidani huku ikilenga kuwajengea uwezo waandishi hao katika kuilewa
tasnia ya mafuta na gesi asilia nchini.
Meneja wa Biashara ya Gesi kutoka TPDC Emmanuel
Gilbert (kulia) akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Mtwara.
Waandishi wa habari kutoa Mkoa wa Mtwara
walioshiriki semina hiyo.
Katibu wa Klabu ya waandishi wa habari
Mtwara Bw. Brayson Mshana akichangia jambo katika semina hiyo.
|
Wawezeshaji wa semina kutoka TPDC wakiwa
katika picha ya pamoja na waandishi
wa habari kutoka Mkoa wa Mtwara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...