Mkuu wa kitengo cha mifumo ya kiteknolojia ya biashara wa Vodacom Tanzania, Josephat Kyando (kushoto)”Head of VAS & M-Commerce Technology” na Meneja wa huduma za M-Pesa wa kampuni hiyo, Polycarp Ndekana wakiangalia moja ya mifumo ya Kiteknolojia inayotumika kutoa huduma za kifedha wakati wa semina ya siku moja ya wafumbuzi wa mifumo mbalimbali ya Kiteknolojia iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa makampuni binafsi ili kujua jinsi gani wanaweza kutumia huduma ya M-Pesa kuboresha biashara zao jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi
ya wafumbuzi
wa mifumo mbalimbali ya Kiteknolojia wa
makampuni binafsi wakiwa kwenye semina ya
siku moja ya wafumbuzi
wa mifumo hiyo iliyoandaliwa na Vodacom
Tanzania ili
kujua jinsi gani wanaweza kutumia huduma ya M-Pesa kuboresha biashara zao
jijini Dar es Salaam jana.
WAFUMBUZI wa mifumo mbalimbali ya Kiteknolojia kutoka makampuni binafsi
jijini Dar es Salaam wamenufaika na mafunzo ya jinsi gani wanaweza kutumia
huduma ya M-Pesa kuboresha biashara zao katika Warsha ya siku moja
iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Akiongea
kuhusiana na mafunzo hayo Mkuu wa kitengo cha mifumo ya kiteknolojia ya
biashara wa Vodacom Tanzania, Josephat Kyando alisema mafunzo haya
ni mafunzo ya kwanza bora yanayoendana na teknolojia ya kisasa ambayo
hayajawahi kutokea hapa nchini yanayohusiana na huduma za M-Pesa ambayo kampuni
imeanza kuyatoa sasa.
Kyando
pia alisema kuwa washiriki wameweza kujua Programu za utekelezaji shughuli za
kibiashara ambazo inaendelea kuzibuni na jinsi zitakavyotumika kuboresha
uendeshaji wa biashara za sekta mbalimbali kupitia huduma ya M-Pesa.
“Hivi
sasa huduma ya M-Pesa imekuwa na inaendelea kutumika katika huduma nyingi za
malipo na kurahishisha biashara na kuwezesha watumiaji wake kuwa na
usalama wa maisha yao na fedha zao hivyo ndio maana tumekuwa na utaratibu wa
kukutana na wadau mbalimbali na kuwaelimisha ni kwa jinsi gani wataboresha
biashara zao kupitia huduma hii”.Alisema.
Alisema
kuwa makampuni mengi binafsi hususani yanayomilikiwa na kuongozwa na vijana
wameonyesha mwamko mkubwa wa kuhudhuria mafunzo haya ambapo pia wanapata fursa
ya kutoa maoni yao kuhusiana na jinsi unavyoweza kuboreshwa zaidi.
Katika
semina hiyo ilibainishwa kuwa huduma ya M-Pesa inaweza kurahisisha na
kuyapunguzia gharama wafanyabiashara na taasisi mbalimbali katika kulipa
mishahara ambapo badala ya kutumia muda mrefu kwenda kwenye mabenki wakawa
wanalipwa kwa kutumia huduma hii ambayo inaongoza kuwa na watumiaji wengi
nchini.
Kyando
alisema kuwa Vodacom kupitia kampeni yake ya Life is Better imedhamiria kubuni
huduma mbalimbali za kutumia mtandao kurahisisha maisha ya watanzania ikiwemo
kuwapatia mawasiliano ya gharama nafuu.





Tunaomba kama mnavyotoa huduma zenu pia mkumbuke kuwalinda watumiaji na mawakala kutokana na wizi kwenye system zenu.
ReplyDeleteWataalamu wenu wngi haswa walioachishwa kazi ndio wanatumia udhaifu wenu kuwaibia mawakala wenu.