Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
TATIZO la utumiaji wa dawa za kulevya kwa  vijana unaanzia  katika shule, hivyo kunahitaji kupimwa wanafunzi wakiwa shuleni katika kuweza kutokomeza tatizo la utumiaji wa dawa hizo.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii jinsia na Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati makabidhiano ya  Gari ya Kituo cha  Kuratibu  Matumizi ya Sumu lilitolewa na nchi ya Japan kwa ofisi ya  Mkemia Mkuu wa Serikali,  amesema kuwa tatizo la utumiaji wa dawa unaanzia shule hivyo ofisi mkemia mkuu wa serikali anaweza kupima wanafunzi kila baada ya muda na kuweza kugundua chanzo cha dawa hizo.
Amesema kuwa wanafunzi wakipimwa kila baada ya muda mkemia anaweza kujua na serika ikaweza kudhibiti juu ya matumizi ya dawa  za kulevya kutokea shuleni.
Waziri, Ummy amesema vijana wanaotumia dawa za kulevya  wengine walianzia katika shule na kuweza kuwafundisha wengine na kuwa ongezeko la watumiaji wa dawa za kulevya na kusababisha nchi kukosa nguvu kazi ya vijana kutokana na kuathirika dawa hizo.
Aidha amesema katika kazi data ya kuweka taarifa za vinasaba vitasaaidia kupunguza watoto wa mitaani kutokana wazazi watambuliwa na vinasaba mara baada ya kupima.
Ummy, amesema kuwa ofisi ya mkemi mkuu wa serikali ni ana kazi kubwa ya kutoa haki kwa kushirikiana na vyombo vingine ikiwemo majanga moto kwa kuweza kutambua watu baada ya kutokea,  vinasaba vya watoto ambao wanakuwa katika mgogoro na kubaini mhusika.
Nae Mtendaji wa Maabara wa Ofisi ya Mkemia Mkuu, Profesa Samwel Manyere amesema kuwa kupata gari hilo watafanya kazi kwa kiwango cha juu kutokana na jinsi walivyojipanga.
Aidha amesema kuwa wameweza kupata cheti cha utoaji huduma kwa kiwango cha Kimataifa (ISO) hivyo kitu chochote kikifanyika kinaendana na viwango hivyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa Waziri;mimi binafsi kama Mzazi nakushukuru sana kwa weledi wako na pia ubunifu wako. wakati unabadilika na mambo pia yanaenda na wakati huo. wakati ule wa zamani ilikuwa hamna mambo ya DRUGS kwahiyo watoto na wanafunzi, haswa wa kike walipimwa mimba! Sasahivi Mheshimiwa kuna mambo ya drugs basi tukupe support kwa hili. Yale yakupima mimba kwa watoto wakike yaendelee na pia upimaji wa matumizi ya drugs yapimwe kwa watoto wote wakike na wakiume. Watanzania wenye weledi kama wako tunakuunga mkono na pia itatusaidia katika kuwatambua watoto wetu. Pia MwenyeziMungu atakuwa nawe na watendaji wenzako daima katika mambo haya mazuri. Go Ummy go. Tuko na wewe Mheshimiwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...