Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania,Evans Lyimo(kushoto)akimuuliza swali Mtaalamu wa masuala ya Saikolojia na Mahusiano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dkt. Chris Mauki(hayupo pichani)wakati alipokuwa akiongea na wafanyakazi wanaume wa kampuni hiyo kuhusiana na jinsi ya kuwekeza kwa mtoto wa kike katika kuazimisha siku ya wanawake duniani jana.
Mtaalamu wa masuala ya Saikolojia na Mahusiano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dkt. Chris Mauki(kulia)akifafanua jambo wakati alipokuwa akitoa elimu kwa baadhi ya wafanyakazi wanaume wa Vodacom Tanzania ya jinsi ya kuwekeza kwa mtoto wa kike katika kuazimisha siku ya wanawake duniani jana.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Mtaalamu wa masuala ya Saikolojia na Mahusiano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dkt. Chris Mauki(kulia)baada ya kutoa elimu kwa baadhi ya wafanyakazi wanaume wa kampuni hiyo ya jinsi ya kuwekeza kwa mtoto wa kike ikiwa katika kuazimisha siku ya wanawake duniani jana.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakimsikiliza Mtaalamu wa Masuala ya Saikolojia na Mahusiano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dkt. Chris Mauki(hayupo pichani)wakati wa kuelimishwa kwa baadhi ya wafanyakazi wanaume wa kampuni hiyo,Jinsi ya kuwekeza kwa mtoto wa kike ikiwa katika kuazimisha siku ya wanawake duniani jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...